Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 30 June 2014

ROSE MUHANDO AIBUKA NA FACEBOOK

IMG_6464roseNa Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili nchini Rose Muhando ameibuka na wimbo mpya uitwao Facebook.
Akizungumza na gazeti hili, Muhando alisema ana imani wimbo huo utakuwa kivutio kikubwa kwa jamii hasa vijana kwa sababu una ujumbe mzuri ambao utagusa wengi.
“Sitaki kuwaambia nimeimba nini, lakini Facebook ni wimbo mzuri na mashabiki wangu naamini wanatambua kwamba mimi si mtu wa masihara ninapotunga kazi zangu,” alitamba mwimbaji huyo.
Alieleza kuwa wimbo huo utakuwa katika albamu yake mpya iitwayo Kamata Pindo la Yesu anayotarajia kuizindua jijini Dar es Salaam katika siku itakayotangazwa wakati wowote kuanzia leo.
Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu msanii huyo ni pamoja na Mteule Uwe Macho, Nipe Uvumilivu, Yesu Nakupenda, Akina Mama, Nakuuliza Shetani, Yerusalemu, Mwambieni Mungu na Nakaza Mwendo.
Pia nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni Kitimutimu, Imani, Onjeni, Sikilizeni Enyi Makahaba, Mungu Wangu, Moyo Wangu, Najitoa Sasa, Hey Mbona Watenda Dhambi na Wapendwa.
Nyingine ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Nyimbo hizo zipo katika albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa na Utamu wa Yesu.
Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya katika albamu ya Vua Kiatu.

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment