Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 27 June 2014

SERIKALI YA JAMHURI YA WATU CHINA YALIKABIDHI SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA (TBC) MSAADA WA GARI LA KURUSHIA MATANGAZO

unnamedNa Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar es Salaam
SERIKALI ya Jamhuri ya Watu imeikabidhi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) msaada wa gari la kurushia Matangazo lenye thamani ya Tsh. Bilioni 6 ili kuboresha utendaji wa shughuli za shirika hilo.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alisema msaada ni kielelezo cha urafiki wa kweli wa kimaendeleo katika nyanja mbalimbali uliopo baina ya Tanzania na China.
Mukangara alisema gari hilo litaisaidia TBC kuteleza majukumu yake kikamilifu na hasa katika kipindi hiki ambacho matangazo mengi ya Televisheni yamekuwa yakirushwa katika mgumo wa dijitali. “Tupo katika mradi kwa kushirikiana na STARTIMES kuhakikisha kuwa TBC inafika katika kona zote za Tanzania na kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri Mukangara.
Kwa mujibu wa Waziri Mukangara alisema Mwezi Oktoba mwaka huu (2014) Rais Jakaya Kikwete atafanya ziara ya kikazi nchini China ambapo pamoja na mambo mengine, Serikali ya China imepanga kuipatia Tanzania mkopo wa liba nafuu ambao utasaidia TBC kujipanga na kufikia malengo yake kwa muda mfupi.
Aidha Waziri Mukangara alisema upo umuhimu mkubwa wa kuimarisha uhusiano wa vyombo vya habari baina ya Tanzania na China kwani kutasaidia kubadilishana utamaduni baina ya nchi hizo mbili. “Kupitia Matangazo ya televisheni tutaweza kubadilisha fikra za jamii zetu na TBC ni lazima iweze kuwa imara katika Nyanja zote” alisema Waziri Mukangara. 
Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alisema msaada huo umekuja katika wakati mwafaka kwani lengo la TBC kwa sasa imejipanga  kikamilifu sekta ya michezo ikiwemo mpango wa kuonyesha matangazo ya moja kwa moja kutoka katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonyesha ulimwengu vipaji vya wanamichezo vilivyopo Tanzania wachezaji waliopo Tanzania.
“Uwanja wa Taifa kwa sasa umekamilifu kwa kiasi kikubwa na hasa katika eneo la mchezo wa mpira wa Miguu, na sisi tumejipanga kuonyesha michezo yote ya mpira wa miguu kuanzia mechi za ndani hadi nje ya nchi’ alisema Mshana.

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment