Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 25 June 2014

NIGERIA YATINGA RAUNDI YA PILI

Wachezaji wa Argentina wakishangilia ushindi wao wa mabao 3-2 dhidi ya Nigeria leo hii mjini Porto Alegre, Brazil.

Na James Truman, brotherdanny5.blogspot

Porto Alegre, Brazil: BAO la Rojo la dakika ya 50 liliwanyima Nigeria sare na pointi muhimu dhidi ya Argentina katika mchezo wa Kundi F dhidi ya Argentina mjini Porto Alegre, lakini halikuweza kuinyima fursa ya kufuzu kwa hatua ya mtoano kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea hapa Brazil.
Ikiwa imepoteza mchezo wake wa kwanza katika fainali za mwaka huu, Nigeria ilijikuta ikifungwa bao dakika ya 3 na mshambuliaji hatari wa Argentina, Lionel Messi, lakini Musa akafanikiwa kusawazisha dakika moja baadaye.
Messi alifunga tena bao la pili dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza, hata hivyo, Musa, mchezaji hatari zaidi katika safu ya ushambuliaji ya Nigeria, aliweza kusawazisha bao hilo dakika ya 47.
Wengi walidhani kwamba hata bao la Rojo la dakika ya 50 lingeweza kusawazishwa kutokana na staili ya 'funga-nirudishe' ya Nigeria, lakini Argentina, ambao wameongoza kundi hilo wakiwa na pointi 9 katika mechi tatu walizocheza, waliweka ngumu.
Kufungwa kwa Iran na Bosnia-Herzegovina kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo ndiko kulikoipa nafasi zaidi Nigeria kuwa timu ya kwanza ya Afrika kusonga mbele wakati mechi nyingine zikisubiriwa usiku huu.
Iran, ambayo iliingia ikiwa na matumaini tele ya kupata ushindi mnono hivyo kuifikia ama kuipita Nigeria yenye pointi 4, ilijikuta ikicharazwa mabao 3-1 na kufungasha virago.
Ivory Coast tayari imekwishafungasha virago kurejea Afrika.

1 comment: