Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 27 June 2014

WASHIRIKI WA FAINALI YA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) WATEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS



 

Washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambao ni washindi wa TMT kutoka kanda sita za Tanzania wakisikiliza maelezo kwa makini kutoka kwa Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers Limited (hayupo pichani)


 Mmoja wa washiriki wa fainali wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambae pia ni mshindi kutoka kanda ya Kati Mkoa wa Dodoma Mwinshehe Mohamed akijitambulisha mbele ya wafanyakazi wa Kampuni ya Kubwa ya Habari ya Global Publishers Limited ambao ndio watengenezaji wa Magazeti pendwa hapa Nchini wakati washiriki hao walipotembelea ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga Mwenge


 Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika majukumu yao ya kila siku


 Washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents wakipewa maelekezo ya jinsi magazeti ya kampuni hiyo yanavyoandaliwa hadi yanaponunuliwa na wadau wa habari



 Maelekezo yakiendelea kwa washiriki wa fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents



Washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publisher mara baada yakutembelea ofisi zao leo zilizopo Bamaga Mwenge Jijini Dar Es Salaam.

Na Josephat Lukaza – Proin Promotions Limited – Dar Es Salaam

Washindi wa Kanda zote Sita za Tanzania wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni washiriki wa Fainali ya Shindano hilo kubwa kabisa nchini na Afrika Mashariki na Kati watembelea ofisi za Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya Risasi, Ijumaa, Uwazi nk ya Global Publishers limited kwaajili ya kujionea jinsi magazeti kutoka kampuni hiyo yanavyoandaliwa mpaka yanapowafikia wasomaji.

Washiriki hao pia waliweza kupata fursa ya kuuliza maswali kwa wafanyakazi hao wa Kampuni ya Global Publishers kwaajili yakufahamu mambo mbalimbali yanayohusu kampuni hiyo Kubwa kabisa Tanzania.

Washiriki wa Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wanatarajia kuingia kambini leo tayari kwa mchakato wa kushindania shilingi Milioni 50 za Kitanzania kwa mshindi mmoja.

Huu ndio muda wa Watanzania kuweza kumchagua mshindi wa Milioni 50 kwa kumpigia kura mshiriki ambae ataonekana kukuna nyonga zao kwa kuonyesha kipaji cha kweli. Watanzania wataweza kuwapigia kura washiriki watakaoonekana kuwa na vipaji kwa kutuma namba za washiriki kwenda namba maalumu itakayotolewa.

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment