Wizara ya Ulinzi nchini Marekani imesema kuwa kundi la kwanza la wanajeshi wa Marekani waliotumwa kulisaidia jeshi la Iraq kupambana na machafuko ya waasi wa kisunni limeanza kazi.
Rais Obama alitangaza juma lililopita kuwa wanajeshi maalum 300, walitumwa Baghdad kuwapa mawaidha na kuwasaidia maafisa wa huduma za usalama, na kuwa takriban nusu ya idadi ya wanajeshi hao tayari imewasili Baghdad katika shughli hizo, na waliosalia wanatarajiwa kuwasili siku chache zijazo.
Wanajeshi 40 wa Marekani walio nchini Iraq ndio kikosi cha kwanza kilichotumwa nchini humo.
Katika siku chache zijazo, wanajeshi wengine kutoka sehemu nyingine za eneo hilo watakua wakiwasili Baghdad.
Utawala wa Obama umekua na kibarua kigumu kueleza kuwa wanajeshi hao hawakua na nia ya kutumika kivita ila lengo lao haswa ni kutoa ujasusi kuhusu hali ilivyo nchini humo.
Serikali ya Iraq ilikuwa imeitisha msaada wa mashambulizi ya angani ya Marekani ili kujaribu kuzuia hatari ya ISIS.
Hata hivyo, rais Obama amesita kufanya chochote kitakacho sababisha shutma za Marekani kuegemea upande mmoja, katika mgongano huo wa kidini.
Mara kwa mara imekua akiitisha suluhisho la kisiasa kwa mgogoro huo, kupitia kwa serikali inayowasilisha vizuri matakwa ya wa Sunni na waKurdi walio wachache.
Hili lisisitizwa siku ya Jumanne na waziri wa mswala ya kigeni wa Marekani, John Kerry, alipoutembelea mji la kikurdi wa Irbl.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment