Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 29 June 2014

UHOLANZI NOMA, MEXICO YANG'OKA KWA MABAO 2-1, WANAWEZA KUKUMBANA NA BRAZIL NUSU FAINALI

Arjen Robben is tackled
Penalti! Robben akienda chini

Uholanzi mwaka huu inaonekana haina masikhara hata kidogo katika fainali za Kombe la Dunia, na kitendo cha kurudia fainali mara tatu bila kutwaa ubingwa kinawaongezea hasira ambapo muda mfupi uliopita wameweza kuing'oa Mexico kwa mabao 2-1 katika mchezo wa mtoano na kufuzu kwenye robo fainali.
Mnyama mbaya wa Uholanzi, Arjen Robben ndiye aliyesababisha bao la ushindi kwa timu yake baada ya kuangushwa kwenye eneo la hatari katika za majeruhi ambapo Huntelaar hakufanya makosa baada ya kuukwamisha mpira wavuni
Mexico ndio walioanza kuliona lango la Uholanzi katika dakika ya 48 kwa bao la Dos Santos, lakini Wadachi hao walipigana kiume hadi dakika ya 88 wakati Wesley Sneijder aliposawazisha mambo.
Penalti ya Uholanzi ililalamikiwa na wachezaji wa Mexico waliodai kwamba Robben alijiangusha, lakini kwa vile refa ndiye mwamuzi wa mwisho, tuta likawekwa na Wadachi hao wakapata bao la ushindi ambalo limewapeleka robo fainali na sasa wanasubiri mshindi baina ya Costa Rica na Ugiriki ambao wanapambana muda huu. 



No comments:

Post a Comment