Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 25 June 2014

IVORY COAST, ITALIA NJE KOMBE LA DUNIA

Matumaini ya Bara la Afrika kuwakilishwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia huko Brazil yalitumbukia nyong'o Ivory Coast iliyokuwa inahitaji sare tu ilikufuzu kwa mkondo wa pili ikiambulia kichapo cha 2-1mikononi mwa Ugiriki.
Kufuatia ushindi huo Ugiriki ilijikatia tikiti ya mkondo wa pili ambapo sasa itachuana na Costa Rica katika mkondo wa pili
Ugiriki ilikuwa ya kwanza kuweka wazi niya yao kupitia bao la kwanza la Georgios Samaras kunako dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinzi wa Ivory Coast Cheick Tiote kupeana pasi bila ya kuhakikisha usalama wake .
Ivory Coast hata hivyo ilifunga bao la kusawazisha kupitia Wilfried Bony aliyetumia vyema pasi safi kutoka kwa Gervinho.
Ivory Coast imetupwa nje na Ugiriki
Ivory Coast itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kusonga mbele kwani walipata nafasi nzuri ya kufanya mashambulizi lakini Salomon Kalou akaboronga .
Hata hivyo bao la Ushindi lilitokana na penalti katika muda wa majeruhi baada ya Giovanni Sio kulaumiwa kwa kumtega mshambulizi wa Celtic Georgios Samaras.
Refarii alipuliza kipenga na mshambulizi huyo akafuma mkwaju kimiani mkwaju uliotamatisha ndoto ya Ivory Coast ya kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza .
Ugiriki ilifuzu kama mshindi wa pili katika kundi C na hivyo sasa itakwaruzana na washindi wa kundi D Costa Rica .
Penalti ya Ugiriki iliyozima Ivory Coast
Colombia ilikamilisha mechi za makundi kwa kuiadhibu Japan 4-1 na kuweka rekodi ya kutoshindwa katika makundi.
Colombia itachuana na mshindi wa pili wa kundi D ambaye ni Uruguay baada ya timu hiyo ya Luiz Suarez kuifungisha virago mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia ilipoilaza 1-0.
Kutokana na kichapo hicho Italia iliungana na uingereza kama timu zilizobanduliwa nje baada ya mkondo wa kwanza .

Aidha Afrika kufikia sasa haina mwakilishi katika mkondo wa pili wa kombe la dunia .
Nayo Italia, bingwa mara nne wa Kombe la Dunia, ilijikuta ikiyaaga mashindano hayo katika hatua ya makundi kufuatia bao la dakika za majeruhi la Uruguay katika mechi iliyokuwa kali na ya kusisimua.
Italia nje ya kombe la dunia .
Hata hivyo habari kuu kutoka katika mechi hii ilikuwa ni kashfa nyingine ya tukio la Luiz Suarez ‘kung’ata’
Mapema katika mechi hiyo, kiungo cha kati wa Italia Claudio Marchisio alikuwa ameonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Egidio Arevalo.Mshambulizi huyo wa Liverpool alionekana kumng’ata beki wa Juventus Giorgio Chiellini dakika moja kabla ya Diego Godin kufungia Uruguay bao la ushindi.
Uruguay sasa itacheza dhidi ya Colombia au Ivory Coast jijini Maracana siku ya Jumamosi katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia, lakini utata unatarajiwa kuibuka kabla ya siku hiyo.
Italia walitoka uwanjani wakiwa na ghadhabu kutokana na waliyoshuhudia kabla yao kuondolewa katika kombe la Dunia la pili bila kupita kutoka mechi za makundi- kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1966.
Kocha wa Italia Cesare Prendelli alisema kabla ya mchezo kuwa ilikuwa “mechi muhimu sana katika taaluma yake kandanda” na baada ya kushindwa akapendekeza kujiuzulu.
Mechi hii ilikuwa na hamaki na hasira ndani na nje ya uwanja.
Baloteli hakuvuma katika mechi hii
Mara kwa mara wasaididizi wa refari walilazimika kuzuia zogo kati ya timu hizo mbili, kipenga cha refarii kikatiza mchezo mara nyingi na wachezaji wakachukua muda mrefu wakisukumana walipokuwa wakikimbia na mpira miguuni.
Italia ilikuwa ikihitaji sare tu ili kufuzu. Katika mfumo wa 3-5-2, Italia walikosa mshikamano, mbio na walihatarisha lango lao kila wakati. Lakini iwapo mfumo wao ulitekelezwa ili kuzuia ushambulizi wa Uruguay, mfumo huo ulisaidia.
Andrea Pirlo alimlazimu mlindalango wa Uruguay Fernando Muslera kuondoa mkwaju wake uliotokana na mpira wa adhabu na kuugongesha mlingoti, huku mshambulizi Ciro Immobile akipiga mkwaju nje ya lango.
Edinson Cavani alitaka kuzawadiwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 50 baada ya kuangushwa na Andrea Barzagli, lakini refarii akapuuzilia mbali.
Refarii huyo raiya wa Mexico hata hivyo angebadili mchezo muda mfupi baadae wakati alipomwonyesha Marchisio kadi nyekundu baada ya kiungo huyo wa kati wa Juventus kumchezea vibaya Arevalo katikati mwa uwanja.
Marchisio alinyanyua mguu na kumgonga kiungo huyo wa Uruguay gotini.
Chiellini akimwonesha refarii alikong'atwa na Suarez
Suarez alikaribia kufunga bao alipopiga mkwaju wa chini kwa chini ambao Buffon aliudaka .
Utata zaidi ulizuka wakati Suarez na Chiellini walipokumbana katika maeneo ya penalti zikiwa zimesalia dakika tisa kwa mechi kukamilika.
Beki huyo wa Italia alilalamika wakati huo huo kwa refarii kwamba alikuwa ameng’atwa na akajaribu kumwonyesha alama.
Wakati wachezaji wa Italia walipokuwa wakiendelea kulalamika, Uruguay wakapata kona.
Suarez alipiga pasi nzuri naye Godin akafunga bao hilo la ushindi.
Itali walijaribu kila wawezalo ili kupata bao, hadi mlindalango Buffon kujaribu kutafuta bao kutokana na kona waliyopata waitaliano dakika za mwisho, lakini upande wake Oscar Tabarez ukawadhibiti.
Hata hivyo huenda mechi hii isikumbukwe sana. Macho yote, kwa mara nyingine yatamwelekea Suarez.
BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment