SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR (ZECO)
Namba yetu
Maulizo: 024 223 8321
Dharura: 024 223 0232
Afisi Kuu
S.L.P 235,
Zanzibar – Tanzania
Simu: +255 774 334 455
Barua Pepe: zeco@zeco.co.tz
TAARIFA KWA WANANCHI WA ZANZIBAR JUU YA KUKATIKA KWA UMEME
Shirika
la Umeme Zanzibar (ZECO) limesikitishwa sana na kuzorota kwa shughuli
za maendeleo kutokana na kukatika kwa umeme visiwani Unguja na Pemba
kuanzia majira ya saa moja usiku hadi saa tatu usiku.
Sababu iliyopelekea kukatika huko ni kutokana na kuondoka kwa gridi ya taifa ambayo Zanzibar inapata umeme kupitia gridi hiyo.
Maeneo
yote ya Unguja na Pemba yalikosa umeme na baadhi ya mikoa mingi ya
Tanzania Bara iliyounganishwa na Gridi ya taifa nayo ilikosa umeme
ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Mengineyo.
Wakati
akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesim Mramba amesema
ya kuwa kuzimika kwa mitambo ya kuzalisha umeme ghafla ndiko
kulikopelekea kukosekana kwa umeme nchi nzima ambako husababishwa na
kuzimika kwa moja ya mitambo ya kuzalisha umeme.
Katika
taarifa yake amefafanua ya kuwa chanzo hasa kilichopelekea kuzimika kwa
mitambo hiyo bado hakijajulikana na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa
kutambua kilichosababisha katizo hilo.
Kwa
upande wa Shirika la umeme Zanzibarlinasikitishwa na kukatika kwa umeme
huko kwani shughuli nyingi za kimaendeleo ziliweza kusimama ikiwemo
wananchi kukosa kutazama na kusikiliza maelezo ya moja kwa moja kutoka
Baraza la Wawakilishi, kukosa kuangalia michezo ya kombe la dunia na
kusimama kwa shughuli nyengine za kimaendeleo.
Shirika
litaendelea kutoa taarifa za kina kwa vyanzo vyovyote vile vya kukatika
kwa umeme na kuwaomba wananchi kuwa wastahamilivu wakati wa matukio
kamahayo yanapotokea kwani husababishwa na mambo ambayo yako nje ya
uwezo wa Shirika.
Shirika linapenda kutoa
kuwakumbusha wananchi kuacha vitendo vya kuhujumu miundo mbinu kwa
kuchimba mchanga chini ya njia za umeme kwani kuanguka kwa nguzo ya
umeme ni chanzo kikubwa kinachopelekea kulikosesha taifa huduma hii
muhimu ya umeme.
Imetolewa na Shirika la Umeme
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment