Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 27 June 2014

MATOKEO YA SENSA YA IDADI YA TEMBO KATIKA MFUMO WA IKOLOJIA WA SELOUS-MIKUMI NA RUAHA-RUNGWA

tembotembo2
Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma matokeo ya sensa ya tembo iliyofanyika mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu ili kuiwezesha Serikali kutambua hali ya rasilimali ya wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya sensa katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.
Matokeo ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi kwa sasa una tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090. Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali.
Takwimu za muda mrefu zinaonesha kwamba mwaka 1976 katika mfumo ikolojia wa Selous–Mikumi kulikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia 22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika kipindi cha mwaka 1984 -1989. Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka na kufikia 70,406 mwaka 2006 baada ya Operesheni Uhai iliyofanyika mwaka 1989 na 1990 na juhudi za kimataifa za uhifadhi ikiwemo kusitisha biashara ya meno ya tembo
Aidha, idadi ya tembo nchini ilipungua hadi kufikia jumla ya tembo 38,975 mwaka 2009 na kuendelea kupungua hadi kufikia tembo 13,084 hivi sasa.
Hali kama hiyo inaonekana pia katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa ambapo sensa ya mwaka 1990 ilionesha kuwa na tembo 11,712 kutokana na wimbi la ujangili. Idadi hii iliongezeka na kufikia 35,461 mwaka 2006. Hata hivyo, idadi hiyo imepungua na kubakia tembo 20,090 hivi sasa.
Kwa matokeo haya inaonesha kuwa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi idadi ya tembo imepungua kwa asilimia 66 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo 38,975. na katika Mfumo ikolojia wa Ruaha–Rungwa Tembo wamepungua kwa asilimia 36.5 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo wapatao 31,625.
Kupungua huku kunathibitishwa na idadi ya mizoga ya tembo iliyohesabiwa wakati wa zoezi la sensa. Jumla ya mizoga 6,516 na 3,496 ilihesabiwa katika mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa. Katika zoezi hili Wizara ilitumia vigezo vya uwiano wa mizoga na tembo hai waliohesabiwa (carcass ratio) kubaini vyanzo vya vifo hivyo. Katika hali ya kawaida, uwiano wa asilimia 7 – 8 unaashiria vifo vya asili kama vile ugonjwa na uzee. Zaidi ya asilimia hiyo inaashiria vifo visivyo vya asili.
CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment