Mratibu wa Mradi wa Kulinda na Kuhifadhi Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST), Godwell Ole Meing'ataki, akizungumza na waandishi wa habari.
Mratibu wa mradi wa kulinda na kuhifadhi maeneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania, Godwell Ole Meing'ataki akiwaonyesha waandishi baadhi ya zawadi zitakazotolewa
Kushoto ni Ofisa Tarafa ya Pawaga Nasson Tumsaidie Mwaulesi, anayefuata ni katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Iringa (IDFA) Juma Ahmed Lalika wakifuatilia kwa makini
Mratibu wa Mradi wa Kulinda na Kuhifadhi Maeneo Yaliyohifadhiwa Kusini mwa Tanzania, Godwell Ole Meing'ataki akiwaonyesha waandishi wa habari vifaa vya michezo.
Baadhi ya zawadi zitakazo tolewa kwenye mashindano hayo.
Mtaalamu wa Mradi wa SPANEST Malima Mbijima akizungumza na waandishi wa habari
Mtaalamu wa Mradi wa SPANEST Edmund Murashani akizungumza na waadhishi wa habari
Na Mathias Canal, Kwanza Jamii-Iringa
Mradi wa kuboresha mtandao wa hifadhi zilizo kusini mwa Tanzania (SPANEST) kwa kushirikiana na Hifadhi ya Taifa Ruaha wameandaa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanaume SPANEST CUP 2014 yatakayoshirikisha Tarafa za Idodi na Pawaga kwa vijiji 21 ambavyo vinapakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa mradi wa kulinda na kuhifadhi maeneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania, Godwell Ole Meing’ataki, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Mashindano hayo ambayo kauli mbiu yake itakuwa ni "PIGA VITA UJANGILI, PIGA MPIRA OKOA TEMBO" yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 28/06/2014 na kumalizika tarehe 08/08/2014 ambapo uzinduzi rasmi utakuwa Julai 5, 2014 katika Tarafa ya Idodi kwa kushindanisha vijiji na vijiji na hatimaye bingwa kupatikana.
Meing’ataki amesema kuwa Mashindano hayo ya mpira wa miguu yameandaliwa kwa mara ya kwanza kwa lengo la kushirikisha kundi la vijana katika Tarafa ya Pawaga na Idodi ambapo mradi wa SPANEST pamoja na Hifadhi ya Taifa Ruaha washirikiana kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi kwa wananchi kupitia mikutano na vikao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau ambao ni vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, magazeti pamoja na kuonyesha sinema za wanyamapori na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Kwa upande wake Ofisa Tarafa ya Pawaga Nasson Tumsaidie Mwaulesi amewasihi wananchi wa Tarafa ya Idodi na Pawaga kushiriki vyema katika mashindano hayo ili kila mmoja aweze kutambua umuhimu wa michezo na kupiga vita Ujangili.
Hata hivyo, kutokana na tatizo la ujangili wa meno ya tembo kukithiri miongoni mwa wananchi na kuanzishwa kwa kampeni mbalimbali za kitaifa katika kupinga ujangili kwa kushirikisha makundi maalumu ikiwemo Operesheni Tokomeza Ujangili iliyoanzishwa na serikali kutambua kwa lengo mahususi la kufichua uovu.
Meng’ataki amesema kuwa wazo la kuunganisha vijana katika vita dhidi ya ujangili bado limeonekana kuwa njia muafaka ya kuutokomeza, kutokana na ukweli kwamba vijana ndio walengwa wakubwa katika kuwashawishi kuingia kwenye maeneo yaliyohifadhiwa na kufanya ujangili, hivyo vita hii itapungua au kumalizika kupitia michezo.
Aidha ameeleza kuwa Lengo la mashindano hayo ni kuunganisha vijana katika vita dhidi ya uharibifu wa mazingira na Ujangili wa wanyamapori (TEMBO), kujenga uelewa juu ya uhifadhi wa wanyamapori miongoni mwa jamii ya vijiji jirani, kujenga mitazamo chanya juu ya uhifadhi wa wanyamapori, kuinua vipaji kwa vijana wanaoishi jirani na hifadhi, kutoa burudani kwa jamii inayoishi karibu na hifadhi.
Takwimu za ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa zinaonyesha kuwa vijana wengi hukamatwa katika matukio ya ujangili kutokana na kulubuniwa na watu wenye fedha kutoka maeneo malimbali nchini kwa kuwapa fedha ili wafanye ujangili kwa wanyamapori kama vile Tembo na wanyama wenngine.
Kwa upande wake Mtaalam wa Mradi wa SPANEST Edmund Murashani alisema kuwa Mashindano hayo yatajikita zaidi katika kuimarisha utalii kwani endapo kama maeneo yataifadhiwa vizuri kipato kitaweza kuongezeka na kuwatoa watu kwenye wimbi kubwa la umasikini nchini Tanzani.
Alisema kuwa Spanest Inafanya jitihada mbalimbali kuhamasisha watu kutambua umuhimu wa Wanyamapori na kupambana na ujangili, hivyo kwa kuanzisha michezo hiyo itakuwa ni njia sahihi kwa vijana na wananchi wanaishi karibu na maeneo ya hifadhi kupata ujumbe kwa njia ya kuburudani na kuimarisha afya za zao.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kuhusu michezo ya wanawake na namna ambavyo watafikisha ujumbe Meng’ataki alisema kuwa hii ni hatua ya kwanza kabisa kwa Spanest kuanzisha mashindano haya, hivyo michezo mingine itaongezeka kutokana na utaratibu utakaowekwa kwa kuanzisha michezo kwa ajili ya Wanawake.
Amesema kuwa ili kuhakikisha ujumbe unafika kwa wananchi ni pamoja na kushirikisha Wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vyombo vya habari, viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali na taasisi binafsi, Wadu wa UNDP, uongozi wa ngazi za juu TANAPA ikiwa ni pamoja na kuwafahamisha watu kuhusiana na Umuhimu wa Wanyamapori hususani Tembo ambapo mashindano mengine yajayo yatakuwa na ubora zaidi.
Naye Katibu wa chama cha miguu Wilaya ya Iringa (IDFA) Juma Ahmed Lalika ametoa pongezi zake kwa SPANEST kwa kuanzisha mashindano hayo katika Wilaya yake Na kuongeza kuwa mashindano hayo yatachezwa kwa mujibu wa sheria kumi na saba za mpira wa miguu,na kufanyika katika mtindo wa ligi ambapo timu zitakazoongoza Kutoka Idodi na Pawaga ndizo zitatinga fainali.
Amesema usajili unaendelea kufanyika ili kuepusha mchezaji mmoja kucheza kwenye timu zaidi ya moja kwani ligi itahusisha vijana wa Tarafa ya Idodi na Kata ya Pawaga pekee na wala sio vijana kutoka kata zingine.
Akitoa ufafanuzi wa lengo la kumuokoa Tembo Mratibu wa mradi wa kulinda na kuhifadhi maeneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania, Godwell Ole Meng’ataki amesema kutokana na idadi ya tembo kupungua kutoka idadi ya zaidi ya Tembo 70,000 na kufikia karibu 13,000 hadi 14,000 kwa mwaka huu, ikiwa ni pamoja na matukio ya ujangili kuongezeka na watu wengi zaidi kukamatwa na meno ya Tembo.
Hata hivyo amesema tembo ana nafasi kubwa sana katika hifadhi kutokana na chakula anachokula, jinsi navyotumia nguvu zake, kinyesi chake, kuvunja baadhi ya vichaka ambavyo wanyama wengine wanashindwa kufika hatimaye kuweza kuishi, mbali na hayo pia ni fahari ya nchi yetu kwani ni rasilimali kubwa ambazo zilianzishwa na Baba wa Taifa zinapaswa kulindwa.
Ameongeza kuwa Ili kutunza heshima ya Tanzania katika uso wa dunia lakini pia kufaidika na utalii ambao watu wanakuja kumuona mnyama huyu ni vyema kupiga vita ujangili na kutunza tembo.
“Hapa Tanzania hakuna duka wala soko la tembo lakini wamekuwa wakiuwawa kwa kasi kubwa hivyo lipo soko sehemu mbalimbali za dunia linalosababisha kuuwawa kwa Tembo nchini Tanzania.” Alisema Meng’ataki
Aidha amezitaja zawadi zitakazotolewa kwenye mashindano hayo kuwa ni Kikombe, Medani ya dhahabu, Medani ya fedha, Medani ya shaba, Mipira, seti za jezi, cheti na safari ya kutembelea Hifadhi ya Ruaha.
Amewasihi wachezaji na wananchi wa Idodi na Pawaga kutambua umuhimu wa wanyamapori ambapo wakihifadiwa watatoa fursa mbalimbali za ajira ikiwa ni pamoja na fedha za kigeni, uwekezaji wa hoteli za kitalii, kuuza vyakula kwa watalii lakini pia kutakuwa na mapato kwa hifadhi na kusaidia miradi ya ujirani mwema.
CREDIT: MJENGWABLOG
No comments:
Post a Comment