Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sc umemalizika salama licha ya changamoto kadhaa kujitokeza na sasa zoezi linaloendelea ni kumalizia kuhesabu kura za wagombea wa nafasi za ujumbe.
Kwa nafasi ya Urais, tayari mambo yameshafahamika ingawa taarifa rasmi kutoka kamati ya uchaguzi haijatangazwa.
Evans Elieza Aveva ni rais wa kwanza wa klabu ya Simba kwani matokeo ambayo sio rasmi yanaonesha ameibuka na ushindi mkubwa.
Aveva amepata kura 1461, huku mpinzani wake pekee, Andrew Peter Tupa akipata kura 381.
Wagombea hawa walikuwa na uzito tofauti, kwasababu dalili za Eveva kushinda zilianza siku aliyoenda kuchukua fomu.
Hata hivyo ilionekana kungekuwa na mchuano mkali endapo Michael Richard Wambura angeendelea na uchaguzi.
Nafasi ya makamu wa rais, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Simba katika uongozi unaomaliza muda wake, Geofrey Nyange `Kaburu` kwa matokeo yasiyo rasmi ameshinda nafasi hiyo.
Matokeo rasmi yatatangazwa muda wowote kutoka sasa, endelea kufuatilia mtandao huu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment