TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa
mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997, Kifungu
Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri wa
Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad
Wilson Ngewe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.
Kabla
ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe, alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA
kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya
Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa
Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi
kavu na Majini Tanzania.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment