Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 29 June 2014

SIKU KAMA YA LEO BRAZIL ILIPOICHAPA SWEDEN 5-2 KWENYE FAINALI NA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA 1958

Gilmar_5b7c2.jpg
Pele na Gilmar wakimwaga machozi ya furaha baadaya fainali
Na Daniel Mbega
MASHINDANO ya fainali za Kombe la Dunia bado yanaendelea nchini Brazil na tayari wenyeji wamefuzu hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya matokeo ya 1-1 dhidi ya Chile.
Sasa mabingwa hao wa zamani watakumbana na Colombia kwenye hatua hiyo ya robo fainali itakayochezwa Julai 4.
Lakini siku kama ya leo, Juni 29, ni miaka 56 tangu Brazil ilipotwaa taji lake la kwanza la dunia katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Råsunda, mjini Solna kwa kuwachabanga wenyeji Sweden mabao 5-2.
Mchezo huo uliochezeshwa na Mfaransa Maurice Guigue aliyesaidiwa na Albert Dusch (Ujerumani) na Juan Gardeazabal (Hispania) ulihudhuriwa na mashabiki 51,800.
Sweden ndiyo ilikuwa ya kwanza kupachika bao katika dakika ya nne u ya mchezo baada nahodha Nils Liedholm kumalizia vyema muvu nzuri. Lakini bao hilo halikudumu sana kwani Edvaldo Izídio Neto al maarufu kama Vavá, aliweza kusawazisha dakika tano baadaye. Katika dakika ya 32 Vavá akaongeza bao la pili na kuifanya Brazil iende mapumziko ikiwa inaongoza 2–1.
Dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili, Brazil ikaongeza bao la tatu ambalo lilifungwa na yosso Edson Arantes Do Nascimento maarufu kama Pelé. Aliumiliki mpira na kuzama nao kwenye eneo la penalti, akamvisha kanzu mlinzi na kufumua kombora lililomshinda kipa Kalle Svensson.
Katika dakika ya 68 Brazil ikapata bao la nne kupitia kwa Mário Jose Lobo Zagallo.
Simonsson alipachika bao la pili kwa wenyeji katika dakika ya 80 lakini Pelé akafunga kitabu cha mabao kwa kufunga la tano katika dakika ya 90 na kufanya matokeo ya mwisho kuwa 5-2 kwa Brazil.
Fainali za mwaka 1958 ndizo zinazoshikilia rekodi a mabao mengi yaliyofungwa kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Mechi ya fainali pia iliweka rekodi ya mchezaji mdogo zaidi na mkongwe ambapo Pelé ndiye aliyekuwa mdogo zaidi (akiwa na miaka 17 na siku 249 days) na Liedholm wa Sweden ndiye aliyekuwa mkongwe zaidi (akiwa na miaka 35 na siku 263).
Pia mechi hiyo ina rekodi ya watazamaji wachache zaidi kwenye mechi ya fainali ikihudhuriwa na mashabiki 51,800.
Vikosi vya siku hiyo vilikuwa: Brazil: Gylmar dos Santos Neves 'Gilmar', Djalma Santos, Orlando Peçanha de Carvalho 'Orlando', Hideraldo Bellini (c), Nilton Santos, José Ely de Miranda 'Zito', Waldyr Pereira 'Didi', Manuel Francisco dos Santos 'Garrincha', Mário Zagallo, Vavá, Pelé. Kocha alikuwa Vicente Feola.
Sweden: Kalle Svensson, Orvar Bergmark, Sigvard Parling, Bengt Gustavsson, Sven Axbom, Reino Börjesson, Gunnar Gren, Nils Liedholm (c), Kurt Ham
rin, Lennart Skoglund, Agne Simonsson. Kocha alikuwa Mwingireza George Raynor.

Originally post in Mjengwablog.com

No comments:

Post a Comment