Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben
amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti ya ushindi lakini akasema
alikuwa ametegwa .
Kocha wa Mexico Miguel Herrera
amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea
Uholanzi .
Herrera amesema kuwa Penalti hiyo dakika
tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo haikufaa''hiyo ni njama ya FIFA
kuiondoa Mexico kwenye kinyang'anyiro hicho .
Robben alikunguwa katika eneo la lango
Uholanzi ilipokuwa imesawazisha bao moja kwa moja na ikaisaidia Uholanzi
kuibuka mshindi kwa mabao 2-1 .
Penalti hiyo ilifungwa na Jan-Klaas
Huntelaar
“nataka kwanza kuwaomba radhi mashabiki
wangu kwa kudanganya na kujiangusha ukweli haikufaa '' Robben aliiambia runinga
ya Uholanzi NOS.
''nafikiri kuwa refarii Proenca alifanya
kweli kuashiria penalti akisema kuwa alikuwa ametegwa na nahodha wa Mexico
Rafael Marquez.
Mexico ilikuwa imeongoza hadi dakika ya
88 ya kipindi cha pili kabla Wesley Sneijder kuisawazishia Uholanzi kabla ya
Huntelaar kufunga penalti iliyozua ubishi mkubwa.
Herrera alisema kuwa haikufaa refarii
kutoka ulaya alipewa mechi kati ya timu kutoka ulaya na Marekani ya kusini.
Kwanini FIFA hawakutupa refarii mwafrika
mhindi ama hata refarii kutoka Marekani kusini ?
CHANZO, BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment