Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.
Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.
Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.
BBC
No comments:
Post a Comment