Wadau, amani iwe kwenu.

Hii sasa ni kali ya mwaka. Kama mnavyojua kwa siku za karibuni kuna kundi la wajumbe wapatao 82 wa Baraza kuu la CHADEMA ambao wameongea na waandishi wa habari kueleza mambo kadhaa ndani ya chama hicho. Miongoni mwa hoja walizokuja nazo ambazo kwa hakika ni ukweli mtupu kwa vile hakuna kiongozi hata mmoja aliyejitokeza kukanusha ni pamoja;


  1. katibu mkuu kujilipa zaidi ya million 130 kwa mwaka huku makatibu wake wa mikoa, wilaya na kata wakilipwa shilingi 0

  2. katibu mkuu SLAA kujikopesha zaidi ya Millioni 160 kwenda kumalizia deni la nyumba yake bila kufuata utaratibu wowote wa kukopa

  3. kitendo cha mbowe kutukodishia magari yake kwa mamillioni ya pesa kila tunapotumia, halafu yanapokuwa chakavu anatuuzia FUSSO MBILI chakavu kwa million 600


  4. kitendo cha MBOWE kukiuzia chama VX V8 MBILI ambazo amenunua kwa pesa za chama halafu anazisajiri kwa jina la MBOWE HOTELS.

    Yapo mambo mengi ambayo pia yanahusu ukiukwaji wa katiba ya chama. Wajumbe hao hawakuishia hapo bali wameenda kwa msajili wa vyama vya siasa kutoa malalamiko ya viongozi wao kukiuka misingi ya chama ikiwa ni pamoja na uongozi kushindwa kuitisha Kikao cha Baraza kuu kinyume cha katiba. Kwa mujibu wa Katiba, Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa kufanyika mwezi Februari 2014. Pia wajumbe hao wamepeleka maombi kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuomba kupatiwa nakala ya matokeo ya ukaguzi uliofanywa kwenye chama chao.

    Baada ya Tamko la wajumbe hao, kumekuwa na matamko kadhaa ya mawakala wa Mbowe na Slaa kutaka kupingana na wajumbe hao 82. Hata hivyo, hakuna tamko hata moja limekanusha madai ya wajumbe hao. Sana sana kinachoonekana ni kuendeleza siasa za unafiki na usaliti. Kwani miongoni mwa matamko hayo ya Pro Mbowe na Slaa yamedai kuwa hao si wajumbe halali wa Baraza Kuu na kwamba wengine walishafukuzwa kwenye chama.


    Baada ya kuonekana kuwa mambo yanawaendea Kombo, Mbowe na Slaa walikuwa na kikao pamoja na Wabunge kadhaa na watumishi wa makao makuu. Kikao hicho kimefanyika juzi usiku Mjini Dodoma, Area D nyumbani kwa Freeman Mbowe. Miongoni mwa walioshiriki Kikao hicho ni pamoja na John Mnyika, Ezekiel Wenje, Mchungaji Msigwa na wengine Kadhaa. Inadaiwa pia na Lema alishiriki kikao hicho. Aidha Dr Slaa naye alishiriki kwenye kikao hicho.

    Katika kikao hicho, Mbowe alilalamikia sana kurugenzi yake ya Ulinzi na Usalama kwa kushindwa kukusanya taarifa juu ya mpango huo. Mbowe alisikitishwa na kitendo cha Wajumbe hao kujiorganize tena wengine wakitoka mikoani na kuja kuongea na waandishi wa habari Dar Es Salaam bila ya Kurugenzi hiyo kuwa na taarifa. Mbowe aling'aka na kusema kuwa hiyo intelligence failure iliyojitokeza inatia doa kurugenzi hiyo na chama kwa ujumla na kwamba wamekidhalilisha chama kwa kiwango kikubwa. Aidha, Mbowe alitoa onyo kali kwa Kurugenzi hiyo na aliwatishia kwamba wasipojitathmini vya kutosha, ajira zao zitaota nyasi.

    Kuhusu madai waliyotoa wajumbe hao, Mbowe alisema kuwa madai hayo ni ya kweli ingawa jinsi yalivyoelezwa yameelezwa kipropaganda kwa lengo la kumchafua yeye na Dr Slaa. Hata hivyo, aliiagiza kurugenzi ya Habari kujibu tuhuma hizo kwa haraka na kwa majibu yanayojitosheleza. Amesema kuwa wasipokuwa makini katika kujibu, watakidhalilisha chama badala ya kukijenga.

    Aidha, Mbowe alihoji imekuwaje kikosi kazi chao mitandaoni kimekuwa dhaifu sana katika kujibu hoja kwa wakati. Alisema kuwa ameshuhudia mara kadhaa mada zinazowekwa against na chama au viongozi wa CHADEMA, wana timu hao wamekuwa nyoronyoro kujibu hoja na hata wakijibu, hoja wanazotoa ni dhaifu sana. Hali hiyo alisema imekuwa ikiwaweka wakati mgumu wana kikosi hao na kwa hali hiyo haoni umuhimu wa kuwa na kikosi hicho licha ya kuwapatia vitendea kazi na posho za kujikimu ambazo hata hivyo hakubainisha aina ya vitendea kazi na kiwango cha posho wanacholipa. Kutokana na hali hiyo, alimuagiza Katibu Mkuu kukiframe upya kikosi hicho ili kiwe na ufanisi zaidi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.

    Naye Katibu Mkuu alionekana kuwa mnyonge sana juu ya masuala kadhaa yanayoendelea ndani ya chama hicho. Dr Slaa alimwambia Mwenyekiti wake kuwa chama hakipo salama na jitihada kadhaa zinatakiwa kuchukuliwa ili kukinusuru. Moja ya Mkakati aliopendekeza Dr Slaa ni kutuma kikosi cha Ujasusi kukutana na wajumbe waliotajwa kwenye ile orodha ya wajumbe 82 wa Baraza Kuu. Hata hivyo, Dr Slaa alitahadhalisha kuwa suala hilo lifanyike kwa umakini mkubwa bila ya kuumbuka. Dr Slaa alimshauri Mwenyekiti kuidhinisha kiasi kikubwa cha fedha, zaidi ya shilingi milioni 300 ili kuwapoza baadhi ya wajumbe hao ili hatimaye wawakane akina Athuman Balozi. Tayari Majasusi wa CHADEMA wameanza kazi yao na kuna mjumbe ameshaonesha usaliti wake kwa wajumbe wenzake. Pia Dr Slaa aliagiza kusaka orodha ya wajumbe 50 waliokosekana kutoka kwenye ile orodha ya wajumbe 82 kwani wajumbe ambao majina yao yamewekwa hadharani ni 32 tu.

    Aidha, Dr Slaa alipendekeza baadhi ya think tanks za chama hicho kujipanga ili kutoa matamko mfululizo mbele ya Waandishi wa Habari. Matamko hayo yamepangwa kutolewa Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Tabora.

    Pia Dr Slaa alipendekeza kuitishwa kwa Kikao cha Kamati Kuu kwa lengo la kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza uanachama wale wote waliohusika na mpango huo ovu. Tayari maandalizi ya kikao hicho cha dharura yanaendelea na wakati wowote kinaweza kuitishwa.

    Wadau, hakika yapo mengi ila kwa leo nimewamegea hayo tu. nitaendelea kufanya hivyo kwa kadri hali itakavyokuwa.