Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 4 June 2014

CHADEMA WAMJIBU MWIGULU NCHEMBA


Mwenyekiti wa hamasa wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John David Mwambigije, amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, asiwahadae wananchi kwamba chama hicho 'kitalikomboa' Jimbo la Iringa Mjini.
Akizungumza jioni hii katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa, Mwambigije maarufu kama 'Mzee wa Upako', amesema badala ya kufikiria kulikomboa jimbo hilo, kwanza aende akahakikishe wananchi wa jimbo lake la Iramba Mashariki wanapatiwa huduma bora za jamii, zikiwemo barabara, hospitali na maji safi ya kunywa.
"Nchemba ameshindwa kuwapatia na kuwapigania wananchi wake ili wapate huduma bora, lakini anapita kila mahali kwa kutumia kodi za wananchi kuipinga Chadema, sasa hili jimbo la Iringa mjini wasiote kama watalipata mwaka 2015," alisema.
Mwambigije, ambaye ndiye aliyekuwa msemaji mkuu kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya watu, aliwataka vijana wa Chadema kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili hatimaye washiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi Oktoba mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
"Jiandikisheni kwa wingi na mgombee nafasi mbalimbali kuanzia kwenye mitaa ili iwe rahisi kuing'oa CCM madarakani mwaka 2015, kama kweli tunataka mabadiliko lazima tushiriki kwa vitendo," alisema.
Naye Mwenyekiti wa Hamasa wa Mkoa wa Iringa, Cecilia Charles Kisyeri, aliwataka akinamama wa mkoa huo kuachana na tabia ya kupokea vitenge, khanga na kofia ili waichague CCM, badala yake waangalie chama gani kinachowafaa kuwaletea maendeleo.
Awali Diwani wa Kata ya Mivinjeni, Nyalusi, alisema CCM haina ubavu wa kushinda jimbo la Iringa Mjini mwaka 2015, kwani Mbunge wa sasa, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amefanya mambo mengi ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment