Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 28 November 2014

MAELFU YA DOLA KUUKARABATI MJI WA BRISBANE

Mvua kubwa ikinyesha jijini Brisbane
Mji wa Brisbane nchini Australia umekumbwa na dhoruba mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Mji huo ulipigwa na mawimbi makubwa na upepo mkali wenye nguvu ya kilomita mia moja na arobaini kwa saa.
Kimbunga hicho chenye nguvu nyingi kimeezua mapaa ya nyumba kadhaa,kuvunja madirisha,matofari yalionekana yakinyanyuliwa na kutupwa na kusababisha nyumba takriban elfu sabini kukosa nishati ,ni mwezi mmoja sasa mvua nyingi zinaendelea kunyesha kila siku kwa nusu saa na hivyo magari yanaonekana yakielea kwenye mitaa iliyofurika maji.
Jeshi nchini humo limeombwa kusaidia kusafisha miji ili kurejea katika hali yake ya kawaida,nayo serikali ya Queensland imekadiria gharama za ukarabati ulisababishwa na kimbunga hicho kwamba huenda ukagharimu mamilioni ya dola za Kimarekani.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment