Watu 78 wameuawa katika mashambulio mawili ya kujitoa mhanga yaliyofanywa sokoni, katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema mlipuko wa kwanza ulitokea wakati washambuliaji hao walipomuwekea mlipuko mwanamke mmoja mwenye matatizo ya akili.
Wakati umati wa watu wakienda kutoa msaada, mwanamke mwingine alijitoa mhanga.
Kundi la kiislamu la wapiganaji la Boko Haram ambalo linadhibiti maeneo mengine ya miji ya kaskazini mwa nchi hiyo na vijiji, linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo.
Mwandishi wa BBC anasema Wanaigeria wamekosa Imani na jaribio la serikali ya nchi yao kufanya mazungumzo na Boko Haram, kutokana an kuongezeka kwa ghasia hizo.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment