Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akimpokea Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 28.4.2014. Mama Salma alikwenda Moshi kuzindua rasmi chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 9 hadi 16.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto, UNICEF, hapa nchini Dkt. Sudha Sharma, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mandela uliopo katika eneo la Pasua katika Manispaa ya Moshi kwa kulikofanyika uzinduzi rasmi ya chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma na vikundi vya kwaya vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16.
Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.
Maandamano ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.
Mamia ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe hiyo.
Mamia ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wanafunzi waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16 huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana kwenye sherehe iliyofanyika huko Pasua, Moshi Mjini tarehe 28.4.2014. Wengine katika picha (kushoto kwenda kulia) ni Ndugu Leonidas Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Rufaro Chatora, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani hapa nchini, Dkt Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila, Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Mama Salma na wa Kwanza kulia ni Mwakilishin wa Shirika la Kuhudumia watoto (UNICEF) hapa nchini Dkt. Sudha Sharma.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwangalia muuguzi akitoa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa msichana Salma Abillah, 12, anayesoma darasa la 4 Shule ya Msingi Azimio huko Moshi mara baada ya Mama Salma kuzindua rasmi tarehe 28.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika taarifa za mtoto Salma Abillah mara baada ya kupata chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na baadaye kumkabidhi kadi yake ambayo anatakiwa kurudi tarehe 28.10.2014 kwa ajili ya kupata chanjo ya pili.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana akitoa chanjo ya matone kuzuia ugonjwa wa polio kwa mtoto Ahmad, miezi 10, aliyefika kwenye sherehe ya uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
CHANZO,FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment