Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 April 2014

IDADI YA WATOTO WANAOZALIWA NA SIKOSELI NCHINI INATISHA

photo1
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani akihojiwa na waandishi wa habari katika hafla ya kuhamsisha jamii kuhusu ufahamu wa ugonjwa wa sikoseli ‘seli mundu’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Ugonjwa  wa sikoseli hurithiwa kutoka kwa wazazi wote wawili wenye.
-Watoto 8,000 mpaka 11,000 kuzaliwa na ugonjwa wa sikoseli
Na Mwandishi Wetu,
TAASISI ya Sikoseli Tanzania imewaomba wadau wengine wa afya nchini kujiunga katika mapambano ya ugonjwa wa seli mundu ‘sickle cell’  kwani idadi ya watoto wanozaliwa na ugonjwa huo kila mwaka inatisha.
sababu utafiti unaonyesha kati ya watoto 8,000 hadi 11,000 kuzaliwa na ugonjwa huo nchi nzima.
Akizungumza wakati wa  kampeni ya kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa ambao iliyoandaliwa  na Mfuko wa  Sikoseli Tanzania (SCFT) na Kituo cha Little Fingers Music mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa SCFT, Dk. Julie Makani alisema kwamba utafiti unaonyesha kati ya watoto 8,000 hadi 11,000 huzaliwa na ugonjwa huo nchini kila mwaka.
Alisema kwamba ugonjwa huo ni wakurithiwa kutoka kwa wazazi baba na mama kwenda kwa mtoto na Tanzania ni nchi ya nne duniani kuwa na wagonjwa wengi wa sikoseli na kama hatapata ufumbuzi wa kukabiliana nao mapemna asilimia tisini na tano ya watoto watakaozaliwa wanaweza kufa kabla ya umri wa miaka mitano.
“nadhani ni wakati muafaka kwa makampuni, wawakilishi wa nchi mbalimbali na wadau wa sekta ya afya kuja kuunga mkono mapambano haya ya sikoseli nchini,’ alisema
Dk. Makani aliongeza kuwa hospital ya Muhimbili wamefungua kitengo maalum kwa ajili ya kuhudumia watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kwa msaada wa mashirika mbalimbali ikiwemo la Welcome Trust kutoka Uingereza ambao wamekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha azma yao.
photo2
Mmoja wa wagonjwa wa sikoseli, Arafa Salim Said, ambaye pia ni muasisi wa Jumuiya ya wagonjwa wa Sikoseli Tanzania (CDPCT) akizungumza kuhusu ni jinsi gani mtu anayeugua ugonjwa huo anaweza kuishi maisha ya kawaida.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Little Fingers Music, Veronica Eyakuze alisema kwamba kituo chake  kinachotoa mafunzo ya kupiga muziki, piano, gitaa na kazi zingine za muziki kwa watoto wadogo wamehamaika kuungana na SCFT  kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo unaotishia uhai watoto.
“sisi katika Little Fingers Music tupo mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo kwa miaka mingi na kusaidia watoto wenye matatizo hayo kwani ni kweli hata  kituoni kwetu tuna baadhi ya watoto wenye sikoseli,’ alisisitiza
Naye Arafa Salim Said (27) mama aliyezaliwa na ugonjwa huo, alisema kwamba ameanzisha taasisi yake ya kupambana ugonjwa huo kwa ajili ya kuhamasisha jamii kwamba ugonjwa huo unaweza kuishi nao bila matatizo yoyote.
“nimeanzisha taasisi yangu ya Wagonjwa waishio na Sikoseli Tanzania katika juhudi zangu binafsi za kuelimisha jamii kwamba ni muhimu kujua mapema na kuweza kuishi na ugonjwa katika maisha ya raha na marefu,” alisema
Arafa alisema kwamba yeye binafsi ameolewa na anaweza kuishi na mumewe bila matatizo yoyote na ana matumaini anaweza kupata mtoto asiye na ugonjwa huo.
Aliongeza pia kwa miaka takribani 10 tangu kitengo cha sikoseli kufunguliwa katika hospitali ya Muhmbili utafiti umeonyesha kwamba vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinapungua.
photo3
Mmoja wa wagonjwa wa sikoseli, Arafa Salim Said akipozi kwa picha na mumewe, Said Msangi ambaye yeye hana sikoseli hafla hiyo. Hiyo ni kuonyesha kuwa mgonjwa wa sikoseli anaweza kuolewa ama kuoa mwenza asiye na ugonjwa huo bila kuleta madhara kwake.
photo4
Mkurugenzi wa Kituo cha Little Fingers Music, Veronica  Eyakuze akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
CHANZO, MOBLOG
 

No comments:

Post a Comment