Papa Francis akiongoza misa ya kuwatangaza John wa 23 na John wa Pili kuwa watakatifu katika kanisa la Mtakatifu Petro ,Vatican.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis Jumapili(27.04.2014) amewatangaza watangulizi wake wawili John wa 23 na John wa Pili kuwa watakatifu mbele ya umati uliofurika uwanja wa kanisa la Mtakatifu Petro,Vatican.
Katu haikuwahi kutokea
kabla kwa papa aliyoko madarakani na yule aliyestaafu kushiriki misa kwa pamoja
hadharani tena katika tukio la kuwatukuza watangulizi wao wawili mashuhuri
kabisa. Kuwepo kwa Benedict ni onyesho la kuweka uwiano ambalo Francis aliliwazia
wakati alipoamuwa kuwatangaza kwa pamoja kuwa watakatifu John na John Paul ili
kuonyesha umoja wa Kanisa Katoliki kuwatukuza mapapa hao wawili ambao walikuwa
wakipendwa na wahafidhina halikadhalika wataka mageuzi.
Francis alishusha pumzi
nzito na kusita kwa muda mdogo kabla ya kutowa tamko la kutangaza utakatifu kwa
lugha ya Kilatin akionekana kama vile ameguswa na tukio hilo la kihistoria
ambalo alikuwa analifanya.
Amesema baada ya
tafakuri, mashauriano na kuomba msaada wa Mungu "tunawatangaza na kuwaelezea
Wabarikiwa John wa 23 na John wa Pili kuwa watakatifu na tutawaorodhesha kuwa
miongoni mwa watakatifu, kuamrisha kwamba watukuzwe kuwa hivyo na kanisa
zima." Shangilio liliibuka kutoka umati ulliofurika kuanzia uwanja wa
Mtakatifu Petro hadi Mto Tiber na kupindukia hapo.
Uwepo wa Benedikt
Benedict alikuwa ameketi
kwenye madhabahu na makadinali wengine na aliwasili mwenyewe kwenye uwanja huo
huku akishangiliwa na umma uliokuwepo akiwa amevalia mavazi meupe na kofia
maalum ya maaskofu. Alisimama kumsalimia rais wa Italia na baadae Papa Francis
wakati alipowasili na aliungana na wenzake kwenye kuimba nyimbo za pamoja za
kidini zilizofuatia ada za kutangaza utakatifu.
Wizara ya mambo ya ndani
ya Italia ilitabiri kwamba watu milioni moja watakuwa wanaiangalia misa hiyo
kutoka uwanja wa Mtakatifu Petro,mitaa inayozunguka uwanja huo na gulio zilioko
karibu ambapo vionyeshoo vikubwa vya TV vimewekwa kuwezesha umati uliokuwa na
shauku kulifuatilia tukio hilo.
Mahujaji wa Poland wenye
bendera nyekundu za nchi hiyo alikozaliwa Papa John wa Pili walikuwa miongoni
mwa watu wa kwanza kufurika kwenye uwanja huo kabla ya hata kuchomoza kwa jua.
Mmojawapo wa raia wa Poland David Halfar aliyekuwepo uwanjani hapo amekaririwa
akisema "Mapapa wanne katika hafla moja ni tukio la shani kulishuhudia na
kuwepo, kwa sababu ni historia inayoandikwa mbele ya macho yetu."
Wengi wa wale waliowasili
mwanzo katika uwanja wa Mtakatifu Petro walikuwa wamepiga kambi usiku kucha
karibu na uwanja huo wakitumia magodoro ya kutia pumzi na matandiko ya kulalia.
Wengine walikuwa hawakulala kabisa na walishiriki katika ibada za mkesha kwenye
makanisa kadha mjini Rome. Benedict aliahidi kuishj maisha ya faragha baada ya
kujiuzulu mwaka jana,lakini Francis alimshawishi awe anashiriki hadharani
shughuli za kanisa.
Benedict alihudhuria
hafla ya mwezi wa Februari ambapo Francis aliwatawaza makadinali wapya
19.Lakini kuhudhuria misa kwa pamoja na Francis ni jambo jengine tafauti
kabisa,kwanza kwa taasisi hiyo ya kanisa iliyoko kwa miaka 2,000 na ni tafakuri
ya shauku ya Francis kuonyesha kuendelea kusonga mbele kwa uongozi huo wa upapa
licha ya kuwepo kwa mvuto tafauti, vitu vya kupewa kipau mbele na siasa
tafauti.
Watakatifu wapya
Papa John wa 23 ambaye
aliongoza kuanzia mwaka 1958 hadi 1963 ni shujaa kwa Waliberali wa Kikatoliki
kutokana na kule kuitisha mkutano wa Baraza la Pili la Kanisa.Mikutano hiyo
imeliingiza kanisa kwenye enzi ya sasa kwa kuruhusu misa ziendeswe kwa lugha za
kienyeji badala ya Kilatin na kushajiisha kuwepo kwa mazungumzo makubwa zaidi
na watu wa dini nyengine hususan Wayahudi.
Wakati wa uongozi wake wa
robo karne kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 2005,John Paul wa Pili alisaidia
kuanguka kwa utawala wa kikomnisti kutokana na kuunga mkono kwake vuguvugu la
Solidarity nchini Poland.Uongozi wake wa kuzuru sehemu mbali mbali duniani na
kuzinduwa Siku ya Vijana Duniani ambayo ni mashuhuri imetowa nguvu kwa kizazi
kipya cha vijana wa Kikatoliki wakati utetezi wake wa mafundisho ya msingi ya
kanisa kumewapa moyo wahafidhina baada ya vurugu za miaka ya 1960.
Therese Andjoua mwenye
umri wa miaka 49 muuguzi ambaye amesafiri kutoka Libreville Gabon na mahujaji
wenzake 300 akiwa amevalia vazi la Kiafrika lenye taswira za watakatifu hao
wawili wapya amesema " John Paul alikuwa matumaini yetu."Amesema hapo
mwaka 1962 alikwenda Gabon na wakati alipowasili aliibusu ardhi na kuwaambia
inukeni,msonge mbele na msiwe na hofu kwa hiyo wakati waliposikia kwa
anatangazwa kuwa mtakatifu wameinuka.
Wafalme,malkia,
marais na mawaziri wakuu kutoka zaidi ya nchi 90 duniani walihudhuria hafla ya
leo.Takriban viongozi 20 wa Kiyahudi kutoka Marekani, Israel,Ufaransa,Italia na
nchi alikozaliwa Papa Francis yaani Argentina na Poland pia walihudhuria hafla
hiyo ikiwa ni ishara ya wazi ya kuthamini hatua kubwa zilizopigwa katika
uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na Wayahudi chini ya John, John wa Pili na
waliowafuatia kutangazwa kuwa watakatifu.
CHANZO,
DW.DE.COM/SWAHILI
No comments:
Post a Comment