Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 April 2014

KOCHA COASTAL KUSAJILI `MAFOWADI` WALIOPANDA HEWANI


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

KOCHA mkuu wa Wagosi wa kaya, Coastal Union, Mkenya, Yusuf Chipo amesema mpira wa miguu ni mchezo wa ajabu kwasababu mwalimu anaweza kuwa na wachezaji wazuri, wanaolipwa vizuri na wanaishi mazingira mazuri, lakini timu ikazidi kufanya vibaya.
Akihojiana na mtandao huu kwa njia ya simu kutoka kwao nchini Kenya alipo kwa mapumziko, Chipo amesema Coastal ina wachezaji wazuri, lakini kuna tatizo la kutojituma kwa wachezaji.

“Unajua Kenya wachezaji wanajituma sana na kuisaidia timu tofauti na Tanzania”
“Pia kwa Kenya waamuzi wana viwango vuzuri zaidi, unapokuja kwa Tanzania marefa wanaboronga sana hasa kwenye mechi muhimu”
“ Nimekuwepo katika ligi ya Vodacom, lakini huwa nashangaa kwanini wachezaji wanakuwa wazembe kwa kiasi kikubwa”.

Aidha, Chipo amekiri kuwa Tanzania ina vipaji vingi vya soka kuliko Kenya, lakini kinachokosekana ni malengo kwa wachezaji na maandalizi kwa ujumla.

“Kila mchezaji anayempata anajua mpira. Ukienda Mbeya unawapa wachezaji wazuri, ukienda Kagera kuna wachezaji wazuri”.

“Kinachoonekana kwa wachezaji ni kushindwa kujitambua kuwa mpira ni ajira. Pia wanakosa mazoezi ya kiufundi na kuwajenga katika saikolojia ya kuutumikia mpira”. Alisema Chipo.
Akiizungumzia klabu yake ya Coastal Union, Chipo amesema kufanya vibaya kwa klabu hiyo ni yeye kutohusika katika usajili wa wachezaji.

Chipo alisema wachezaji waliosajili Coastal walikuwa katika mipango ya kocha aliyepita kwasababu kila mwalimu ana mfumo wake na matarajio yake.

“Mimi nilikuja na kupewa wachezaji ambao nilitakiwa kupambana kulingana na vipawa vyao. Pili ndani ya klabu tuna matatioz yetu ambayo yanaathiri wachezaji”.

“Tukizungumzia ligi ijayo, mimi nina fursa. Nitatafuta wachezaji wawili watatu kulingana na falsafa yangu na maono yangu”.

“Mimi napenda sana kupiga mipira mirefu, hivyo nahitaji washambuliaji warefu. Nitawatafuta na nitafanikiwa msimu ujao”. Alisema Chipo.

Hata hivyo, Chipo aliwashauri makocha wa Tanzania kuwa na msimamo mkali na kuzingatia falsafa zao.
“Kila mwalimu ana mfumo wake wa ufundishaji”
“ Linapokuja suala la viongozi wa klabu kuwa na matakwa yao tofauti na falsafa ya mwalimu, hapo ndipo utajua yupi mwalimu bora”.

“Kitu cha msingi ni kutambua kuwa ukocha ni taaluma, kuna miiko ya mpira tunayojifunza sisi kama walimu”.

“ Ni wajibu wetu kuwa na msimamo na kuepuka kushinikizwa kufanya mambo kinyume na falsafa zetu”. Alisema Chipo.

CHANZO, MPENJABLOG

No comments:

Post a Comment