Na Zainab Maeda, Iringa
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Pindi
Chana amewaagiza viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kukusanya takwimu
kamili za watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.
Pindi alitoa agizo hilo juzi katika siku ya sikukuu ya
pasaka wakati aliposhiriki katika hafla fupi ya chakula cha mchana na
watoto yatima na wanaishi katika mazingira magumu katika Kanda ya Mlandege
Manispaa ya Iringa, iliyoandaliwa na Diwani wa Viti Maalum wa Kanda hiyo
Dora Nziku.
“Tupewe takwimu za watoto wanaoishi katika mazingira magumu
na yatima pamoja na watoto wa mitaani, takwimu hizi zitatusaidia kufahamu
watu hao kwa haraka zaidi na namna ya kuwashughulikia,” alisema Pindi na kuongeza:
“Watendaji wa Serikali za Mitaa ni wajibu wenu wa
kuwatambua watoto wetu walio yatima au wanaoishi katika mazingira magumu na
hatarishi kwa maisha yao pamoja na watoto wa mitaali ili wasaidiwe.”
Alisema kuwa watoto wamekuwa wakinyanyasika sana na mila na
desturi zilizopo katika baadhi ya familia za Watanzania.
Mbali na kusema hayo aliwataka wazazi na walezi kuwajali
watotot kwa kuwapa lishe bora ili wawe na afya bora.
Naye mwandaaji wa hafla hiyo Diwani Dora aliwataka Watanzania
kuwa na mioyo ya huruma kwa watotot kama hawa kwa kutoa chochote walichonacho
kwa kuwa kutoa ni moyo na sio utajiri.
“Ndugu zangu watoto hawa ni wakwetu tunapaswa kujua
nakufahamu wanavyoishi kwa Yule mwenye moyo wa kutoa tuwe tunawakumbuka
watoto hawa ili wajiskia kuwa wapo sawa na wengine, nataka kuwaambia kuwa kutoa
ni moyo na sio utajiri,” alisema Dora.
No comments:
Post a Comment