Hali shwari sasa!. Mshambuliaji wa Manchester United, Mholanzi, Robin Van Persie ameamua kuendelea kukaa katika klabu hiyo kufuatia kufukuzwa kwa David Moyes.
Kilichomvutia zaidi nyota huyo ni klabu hiyo ya Old Trafford kutaka kumleta Mholanzi mwenzake, Louis Van Gaal kurithi mikoba ya ukocha mkuu.
Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa Van Gaal tayari ameshakubali vipengele vya mkataba saa 48 zilizopita ili kuwa kocha wa kudumu wa Man united.
Sio siri kuwa Van Persie amekuwa na mahusiano mazuri na kocha wake wa timu ya taifa na sasa anaona itakuwa jambo zuri kukaa pamoja Old Trafford baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Taarifa za ndani ni kuwa kocha huyo wa Uholanzi na nahodha wake RVB wanatumia wakala mmoja, bwana Kees Vos ambaye kwasasa yupo katika vikao vya makubaliano ya kazi mpya baina ya Van Gaal na Man United.
Van Persie alikuwa akihusishwa kuihama Man United majira ya kiangazi mwaka huu kwasababu klabu yake imeshindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa katika msimu wake wa kwanza ambao alibeba taji chini ya Sir Alex Ferguson.
Pia kulikuwa na hali ya kutoelewa na bosi wake David Moyes kwa madai kuwa mbinu za ufundishaji za Mscotish huyo zilikuwa haziendani na mfumo wa uchezaji wa Van Persie.
Lakini nahodha huyo wa zamani wa Asernal ameamua kukaa Man United hata kama klabu inatarajia kusaka mshambuliaji mwingine wa kati kwa sababu bosi wake anakuja.
CHANZO, MPENJABLOG
No comments:
Post a Comment