Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru kuwaongoza watanzania katika maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka Aprili 26 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Aprili 26 mwaka 1964, Watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo wakiwemo marais wa nchi mbalimbali za Afrika, Viongozi mbalimbali na wawakilishi wa nchi katika mataifa mbalimbali ya Afrika, Nchi za kiarabuni, Asia na Ulaya, Fullshangwe ilikuwepo kwenye eneo la tukio na kukuletea moja kwa moja matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika maadhimisho hayo ambayo yamefana kwa kiwango kikubwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA UHURU)
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Yoweri Mseveni wa Uganda katikati nI King Mswati wa Swaziland na kushoto ni Rais Piere Nkurunzinza wa Burundi.
Rais Jakaya KIkwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya katikati ni Rais Piere Nkurunzinza wa Burundi na kushoto ni Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais Uhuru Kenyata mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru.
Rais Piere Nkurunzinza akisalimiana na Rais mstaafu wa Zambia Mh. Rupia Banda wakati wa maadhimisho hayo, katikati ni Rais Mstaafu wa Namibia Dr. Sam Nujoma.
Kikosi cha Makomandoo kikionyesha ukakamavu na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete.
Ni maumbo mbalimbali yaliyoonyeshwa na watoto wa halaiki wakati wa maadhimisho hayo.
CHANZO, FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment