Wadau wa sekta ya Usafiri wa anga nchini ,wamekutana katika warsha ya siku moja kujadili rasimu ya mpango kamambe wa usafiri wa anga yaani ( the Civil Aviation Master Plan) makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini(TCAA), Banana-Ukonga.
Warsha hiyo iliyowakutanisha wadau kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga nchini , Mamlaka ya Viwaja vya Ndege na mwenyeji Mamlaka ya Usafiri wa Anga imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho.
Lengo la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri wa anga nchini ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya Dunia. Kampuni hiyo ilianza kuanda rasimu hiyo mwaka 2015 kazi ambayo imefanyika kwa miezi 12.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo , katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema lengo la serikali ni kuwezesha Tanzania kutoa huduma za usafiri wa anga kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubaliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) pamoja na kuweka mazingira mazuri yatakayoruhusu ushindani wa kibiashara katika sekta hii.
Ameongeza kuwa sekta ya usafiri wa anga imekuwa ikikua , mathalani takwimu zinaonyesha safari za ndege zimeongezeka kwa asilimia 8 katika mwaka 2015 ikilinganishwa na zile zilizofanyika mwaka 2014. Kadhalika idadi ya abiria imekuwa ikikua kwa kiwago cha asilimia 1.5- 2 kwa mwaka.
Lengo la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri wa anga nchini ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia chini ya udhamini wa Benki ya Dunia.
Captions
01.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi George Sambali (kushoto) wakiwa kwenye warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) warsha hiyo ilifanyika katika ofisi za Makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
0.Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho akifungua warsha ya kujadili rasimu ya Mpango Kamambe wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) iliyofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA). Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
03.Baadhi ya wadau mbali mbali wa sekta ya usafiri wa anga wakishiriki warsha ya kujadili rasimu ya Mpango wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil Aviation master Plan) uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Banana - Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment