Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Brigedi
Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki, kabla ya kufanya
mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Kulia ni Kamishna
wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar, Ali Abdalla Maalimmosi. Waziri
Kitwanga yupo Zanzibar kwa kwa ziara ya kikazi ya kuangalia hali ya uimarishaji
wa usalama visiwani humo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Wakuu wa
Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Waziri Kitwanga aliwataka wakuu
hao kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unazidi kuimarishwa katika
maeneo mbalimbali ya visiwani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi mjini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
Brigedi
Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki (kulia)
akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
(katikati) wakati wa kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar
na Waziri huyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto
na Uokozi, Zanzibar. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari mjini Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya
Ulinzi na Usalama visiwani humo. Waziri Kitwanga amewataka wananchi wajitokeze kwa
wingi siku ya uchaguzi Machi 20, 2016 bila kutishwa na mtu yeyote, na kila
mwananchi aondoe hofu siku hiyo kwani vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kwa
ajili ya kuusimamia uchaguzi huo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi
****************************************************************************
Na Felix Mwagara (MOHA)
WAZIRI wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amewataka wananchi wa visiwani
Zanzibar kujitokeza kwa wingi Machi 20, 2016 ili waweze kupiga kura kwa amani
na utulivu bila kubughudhiwa na mtu yeyote.
Kitwanga
amesema kuwa ulinzi umeimarishwa na kuwataka wananchi visiwani humo kujitokeza
kwa wingi kuja kumchagua kiongozi wanaompenda siku ya uchaguzi huo na watarejea
nyumbani kwao salama mara baada ya kumaliza kupiga kura.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Maafisa Waandamizi
wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na baadaye kuzungumza na
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Waziri Kitwanga alisisitiza kuwa, vyombo
vya ulinzi na usalama vimejiandaa vizuri na wananchi waondoe shaka kwani
hawatakubali vurugu ya aina yoyote itokee.
“Jitokezeni
kupiga kura siku ya uchaguzi kwani ni haki yenu, nawahakikishia usalama upo na wa
hali ya juu, asijitokeze mtu yeyote akawatisha kutokuja kupiga kura,
tumejipanga vizuri na lengo letu kubwa kabisa ni kuwalinda wananchi,” alisema
Kitwanga.
Hata
hivyo Waziri Kitwanga alisema hakuna mwananchi yeyote anayehama kwakuogopa
vurugu siku ya uchaguzi bali watu wanasafiri kwasababu mbalimbali ikiwemo hiki
ni kipindi cha maandalizi ya Sikukuu ya Pasaka, baadhi ya wananchi wanaenda kula
sikukuu maeneo mbalimbali nchini na wengine wanasafiri kutokana na majukumu
mbalimbali na sio wamekuwa wakimbizi wakikimbia sehemu zao kama inavyoenezwa.
“Acheni
kusikia habari za mitaani amani ipo, jitokezi kupiga kura na hii habari mnayosikia
eti watu wameanza kuyakimbia makazi yao ni uzushi tu, hakuna kitu kama hicho,
wananchi wanaendelea na shughuli zako kama kawaida na vyombo vya ulinzi
vimejipanga kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zao,” alisema
Kitwanga.
Waziri Kitwanga
amewasili Zanzibar leo kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kuimarisha usalama zaidi visiwani humo pamoja na kujua mikakati
iliyowekwa na vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu usimamizi wa uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment