Mtendaji Mkuu wa
kampuni inayotoa huduma za simu Benoit Janin wa pili kutoka kushoto akiongea na
wanahabari hawapo pichani katika hafla ya kuwakabidhi msaada wa komputa tatu
kituo cha Mkubwa Fella. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi Idara ya Maendeleo
ya Sanaa Wizara ya Habari. Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi Hafla
hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari. Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah
Kihimbi wa pili kutoa kushoto akikabidhi msaada wa Komputa tatu kwa wawakilishi
wa Mkubwa Fella wa kwanza kulia ni Bw. Yusuph Chambuso.
Baadhi ya wasanii wa
kikundi cha Yamoto Bendi wakionyesha umahiri wao wa kuimba mbele ya wanahabari
wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa kompyuta tatu kwa kikundi cha Mkubwa
Fella iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Benjamin Sawe).
Benjamin Sawe.
WHUSM.
Wananchi wametakiwa kuupenda,
kuuthamini na kuuendeleza utamaduni kwa kutumia Sanaa kwani utamaduni ni mali
ya jamii.
Hayo yamesemwa leo (jana) na Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Wizara ya Habari. Utamaduni, Sanaa na Michezo
Bi. Leah Kihimbi katika hafla ya kukabidhi msaada wa Komputa tatu zilizotolewa
na kampuni ya huduma za simu ya Zantel kwa mlezi wa Kikundi cha Fella na Wanawe
iliyofanyika jijjini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Bi.
Kihimbi alisema kazi inayofanywa na kituo cha Mkubwa Fella ni utekelezaji wa
Sera ya Taifa ya utamaduni inayosisitiza ukuzaji wa sanaa katika kuendeleza na
kuongeza maslahi ya wasanii.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Zantel
Mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin alisema sanaa ni ajira kama zilivyo ajira
nyingine hivyo anaamini msaada huo utawawezesha vijana wengi kuboresha na
kusambaza zaidi kazi zao za sanaa hivyo kuweza kujikimu kimaisha na kutoa ajira
kwa wengine.
Akizungumza kwa niaba ya mwanzilishi wa
kituo cha Mkubwa Fella Bw. Yusuph Chambuso alisema Mkubwa na Wanawe imejikita
kujenga na kuhakikisha vijana wanatimiza ndoto yao na kuwasaidia wasishawishike
au kujishughulisha na shughuli haramu ambazo zinapotosha maadili kwenye jamii.
Kituo cha Mkubwa na Wanawe ni kituo cha
kukuza sanaa, kilichoanzishwa mwaka 2011 katika Wilaya Temeke kwa lengo la
kufanya maonyesho ya sanaa na kutoa fursa kwa vijana wanaoishi kwenye mazingira
magumu kuweza kukuza na kuviendeleza vipaji vyao.
Tangu kuanzishwa kwake, Mkubwa na
Wanawe imefanikiwa kuibua wasanii mbalimbali kama vile Wanaume TMK na bendi ya
Yamoto ambapo mpaka sasa kituo hicho kinaidadi ya vijana 102 ambao wana vipajji
mbalimbali kama vile kuigiza, kuimba na kucheza ngoma.
No comments:
Post a Comment