Na Deodatus Kazinja-PHQ
Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limetiliana Mkataba wa uwekezaji na Mfuko wa Jamii wa GEPF ambapo majengo ya vitega uchumi yatajengwa katika maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Tukio hilo la utiwaji sahini mkataba huo limefanyika leo Alhamis 29, 2014 katika ukumbi wa mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es salaam. Akiongea katika hafla hiyo Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja amesama ni kiu yake kuona mradi huo unaanza kutekelezwa ifikapo Julai Mosi, 2014. Naye Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw. Daud Msangi amesema ukiwepo ushirikiano wa kutosha miradi hii itaweza kukamilika mapema iwezekanavyo kwa faidi ya pande zote mbili.
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment