Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 30 May 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

0
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF                                                   
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF NI MFUKO WA HIFADHI YA JAMII NCHINI TANZANIA WENYE MAKAO MAKUU YAKE MJINI DODOMA.
MFUKO WA PENSHENI WA LAPF UNAENDESHWA CHINI YA SHERIA YA LAPF(THE LOCAL AUTHORITIES PENSIONS FUND ACT NO. 9 OF 2006). SHERIA HII IMEFANYIWA MAREKEBISHO KUKIDHI MAHITAJI YA SHERIA YA USIMAMIZI WA HIFADHI YA JAMII YA MWAKA 2008 (SSRA) NA KWA SASA LAPF INAANDIKISHA WANACHAMA TOKA SEKTA ZOTE NCHINI NA JINA LA MFUKO LILIREKEBISHWA NA SASA LINAJULIKANA KAMA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF(LAPF PENSIONS FUND).
SHUGHULI KUU ZA MFUKO NI PAMOJA NA KUANDIKISHA WANACHAMA, KUKUSANYA MICHANGO, UWEKEZAJI NA KULIPA MAFAO. KWA SASA LAPF INATOA MAFAO MBALI MBALI AMBAYO NI MAFAO YA UZEENI, MAFAO YA MIRATHI, MAFAO YA KUUMIA KAZINI, MAFAO YA UZAZI, MAFAO YA KUJITOA, MSAADA WA MAZISHI, MIKOPO YA NYUMBA, MIKOPO YA WANACHAMA KUPITIA SACCOS NA IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUTOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA.
PAMOJA NA MAJUKUMU MAKUU YA MFUKO YALIYOTAJWA HAPO JUU, MFUKO UNASHIRIKI PIA KATIKA KUISAIDIA JAMII NA HIVYO KUSAIDIA KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUCHOCHEA MAENDELEO ( CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY). UTARATIBU HUU NI WA KAWAIDA KWA MASHIRIKA YOTE YA HIFADHI YA JAMII, TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA NA MASHIRIKA BINAFSI KAMA SEHEMU YA UTAWALA BORA.
MISAADA HII INA LENGO LA KUSAIDIA JAMII YOTE YA WATANZANIA YENYE MAHITAJI MBALI MBALI NA KWA KUTAMBUA KUWA MISAADA HII ITAWANUFAISHA SI WANACHAMA WA LAPF TUU BALI PIA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA.
LAPF IMEKUWA IKITOA MISAADA YA KIJAMII KATIKA SEKTA MBALI MBALI KAMA VILE AFYA, ELIMU, VITUO VYA WATOTO YA YATIMA, TAASISI ZA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM, SEKTA YA MICHEZO NA KUSAIDIA KATIKA MATUKIO YA MAAFA.
KATIKA SEKTA YA AFYA, MATUKIO YA MAAFA NA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA, LAPF IMEKUWA IKITOA MSAADA WA CHAKULA NA VIFAA MBALIMBALI KAMA VYANDARUA, MAGODORO, SHUKA, DAWA NA VIFAA VYA MAABARA.
KATIKA SEKTA YA ELIMU MFUKO UMEKUWA UKICHANGIA MADAWATI, MABATI, SARUJI, TAA ZINAZOTUMIA NGUVU YA JUA NA MASHINE ZA KUDURUFU NYARAKA. KATIKA MICHEZO MFUKO UMEKUWA UKICHANGIA VIFAA MBALIMBALI KAMA MIPIRA NA JEZI.
KWA MFANO KATIKA MWAKA HUU WA FEDHA, MFUKO UMECHANGIA VIFAA VYA UJENZI KWA CHUO CHA MADAKTARI BUGANDO NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA (OUT). PIA MFUKO UMEENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA MICHEZO KWA SHIRIKISHO LA SERIKALI ZA MITAA (SHIMISEMITA) NA MICHEZO YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU (TUSA).
HII NI BAADHI TU YA MISAADA AMBAYO LAPF IMETOA KWA KUZINGATIA MAOMBI MBALIMBALI YALIYOWASILISHWA PAMOJA NA BAJETI NA MPANGO WA MFUKO ULIOIDHINISHWA.KWA MWAKA HUU WA FEDHA, MISAADA YOTE HADI SASA INA JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI MILIONI MIA MOJA NA ISHIRINI.AIDHA, KUTOKANA NA UFINYU WA BAJETI YA MFUKO, SEHEMU KUBWA YA MISAADA HII NI KATI YA SHILINGI LAKI TANO HADI MILIONI TATU.MISAADA HII HUTOLEWA MOJA KWA MOJA KWA WALENGWA NA PIA SI FEDHA TASLIMU, BALI VIFAA HUSIKA.
PAMOJA NA MAELEZO HAYO, MFUKO WA LAPF PIA UNAPENDA KUKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUWA LAPF ILITOA MSAADA KWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI NA MBUNGE WA IRINGA MJINI MH. PETER MSIGWA. IELEWEKE KUWA INGAWA WAHESHIMIWA WABUNGE AU MTU AU TAASISI YEYOYE HAWAZUILIWI KUOMBA MSAADA WA KIJAMII, MH. MBILINYI NA MH. MSIGWA HAWAJAWAHI KUWASILISHA MAOMBI NA HAWAJAWAHI KUPEWA MSAADA WOWOTE NA LAPF.LAPF PIA INAKANUSHA HABARI ZILIZOTOLEWA KATIKA GATEZI LA MTANZANIA LA TAREHE 26 MEI 2014 TOLEO NA.7472 KUWA WAHESHIMIWA WABUNGE NI WASUMBUFU NA KUMFANYA MKURUGENZI MKUU ASIENDE BUNGENI.
AIDHA, SI KWELI PIA KWAMBA LAPF HAISHIRIKI KATIKA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KWANI MFUKO HUU UKO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI NA INASHIRIKI KATIKA VIKAO HIVYO.
LAPF INAKANUSHA PIA HABARI ILIYOTOLEWA KATIKA GAZETI LA THE GUARDIAN LA TAREHE 27 MEI 2014 TOLEO NA.6031 KUHUSU KUMKOPESHA MH. FREEMAN MBOWE SHILINGI BILIONI MOJA. IELEWEKE KUWA LAPF HAIJAWAHI KUMKOPESHA MH. FREEMAN MBOWE NA KWAMBA MH. MBOWE ALIKOPESHWA NA MFUKO MWINGINE WA HIFADHI YA JAMII HAPA NCHINI.MFUKO WA LAPF HAUNA UTARATIBU WA KUKOPESHA MTU MMOJA MMOJAHIVYO HAKUNA MIKOPO YA AINA HIYO. LAPF HUTOA MIKOPO YA WANACHAMA WAKE KUPITIA VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA (SACCOS) NA MIKOPO YA NYUMBA KWA WANACHAMA WANAOKARIBIA KUSTAAFU.
LAPF INAPENDA KUUJULISHA UMMA WA WATANZANIA KUWA MFUKO HUTOA MISAADA YA KIJAMII KWA KUZINGATIA MPANGO NA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KWA KUZINGATIA SERA YA MISAADA YA KIJAMII NA MAOMBI YANAYOWASILISHWA. PIA HAKUNA MTU BINAFSIAU TAASISIINAYOPEWA FEDHA TASLIM ISIPOKUWA MFUKO HUNUNUA VIFAA NA KUWASILISHA MOJA KWA MOJA KWA WAHUSIKA.
STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.

CHANZO FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment