Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 23 May 2014

KUMBUKUMBU YA HEMEDI MANETI ULAYA JUNI 6!

Haya 'Chiriku' Hemedi Maneti Ulaya enzi za uhai wake
Stone Lady Kida Waziri

Ndugu zangu,
Mwaka huu tunaazimisha miaka 24 ya kifo cha mwanamuziki mahiri Hemedi Maneti Ulaya 'Chiriku' aliyefariki dunia Mei 31, 1990 majira ya saa 11 jioni katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Kwa vijana wengi waliozaliwa mwaka 1985 kuja juu, jina hili wanaweza kuwa wamelikuta kwenye simulizi tu, hawakuwahi kubahatika kumuona akiimba jukwaani.
Lakini Maneti ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa bendi ya Vijana Jazz tangu mwaka 1973 ikimilikiwa na Umoja wa Vijana wa TANU (sasa CCM) na alidumua nayo kwa muda wa miaka 16 hadi mauti yalipomkuta. Tangu alipojiunga/kuanzisha bendi hiyo akitokea Kilosa Jazz, Maneti hakuwahi kuondoka hapo na alikuwa mbunifu mkubwa akishirikiana na wanamuziki wenzake wengi.
Maskini, alifariki akiwa bado kijana wa miaka 36 tu na hakika akaacha pengo kubwa kwenye bendi hiyo ambayo imefufuka tena upya.
Watoto wake pamoja na wanafamilia hivi sasa wamepanga kufanya onyesho la Kumbukumbu ya Maneti litakalofanyika Juni 6 kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.
Kwa mujibu wa bintiye ambaye ni mwanamuziki, Khomweta 'Khairat' Maneti, onyesho hilo litawahusisha wanamuziki wengi waliopata kuimba na marehemu baba yao wakiwemo akina Kassim Mapili, Anko John Kitime, Rashid Pembe, Shomari Ally 'Shomy Guy', Kida Waziri, Edna Pambamoto na wengineo wengi na litapambwa na bendi mbalimbali zikiwemo Vijana Jazz na Msondo Ngoma.
Hili litakuwa onyesho la kwanza maalum la kumbukumbu ya nguli huyo, ambaye amesahauliwa hata na Umoja wa Vijana wa CCM wenyewe (wengi wa viongozi wake wakiwa miongoni mwa vijana waliozaliwa kuanzia mwaka 1985 na kuja juu - hawamjui).
UV-CCM ilimsahau nguli huyo na wala haikutekeleza ahadi yake iliyotoa wakati wa mazishi yake pale kwenye Kijiji cha Mamboleo, Muheza mkoani Tanga mwaka 1990 kwamba ingewasomesha watoto wa marehemu mpaka chuo kikuu. Lakini Kulwa na Dotto, waliozaliwa na mkewe Chiku wa Sumbawanga, mpaka sasa hakuna anayejua walipo, wakati ambapo Khomweta aliishia kidato cha tatu kwa kukosa ada na kaka yake, Maneti, hakusoma sekondari. Binti yake Cecilia, ambaye alizaa na Kida Waziri, naye hakuuona msaada wowote kutoka UV-CCM. Inasikitisha hasa kwa mtu aliyejitoa kuimba nyimbo za sifa kwa chama.
Hata hivyo, ni wakati muafaka wa Watanzania, hususan familia ya wapenda muziki, kushiriki katika onyesho hilo muhimu ili kuwaunga mkono wanafamilia na huo uwe mwanzo tu wa kuwakumbuka watu walioiletea sifa kubwa nchi yetu.

Ndugu yenu,
Daniel Mbega
Iringa, Tanzania
0656-331974

No comments:

Post a Comment