USHARIKA wa Ngaramtoni mjini Arusha umechangia zaidi ya shilingi milioni moja na nusu katika harambee ya kuchangia kulipa deni la Hoteli ya Dayosisi ya Kaskazini Kati,Corrido Spring ya jijini Arusha.
Katika harambee hiyo iliyofanyika usharikani hapo hivi karibuni Mchungaji Nodfrey Philipo kutoka Chuo Kikuu Cha Tuamaini Makumira(TUMA) alisema suala la utoaji ni la mtu na Mungu wake anayemuamini na ndiyo maana kila mmoja anapeleka sadaka kule anapo paamini.
Pia alisema kuwa wapo wanaoto a sadaka zao kwa waganga wakienyeji na wanapokwenda kutambika kwa sababu wanaamini kuwa huko ndiko mahali sahihi.
Alisema kwa Mkristo safi Kanisani ndipo mahali sahihi pakutoa sadaka, pia ifahamike kuwa utoaji sio kwa ajili ya mchungaji wala watumishiwengine katika kanisa bali ni kueneza injili kila mahali”alisema Mchungaji Philipo.
Alifafanua kuwa kila Mkristo anapaswa kutambua kuwa kadri Mungu anavyoendelea kumbariki na kumtendea mema ndivyo hivyo yampasa amtolee kwa njia ya sadaka iliaweze kumbariki zaidi.
Alisema lakini mkristo akiugua na kupata shida ya kiuchungajaji ndipo ananza kuona umuhimu wa Mchungaji na Kanisa na hata kumjua Mungu ila wakati wa furaha kanisa halinanafasi.
Naye mwinjilisti wa Usharika huo Lamayani Nginuku,alisema kile kidogo ambacho Mungu amekupatia ndicho unachopaswa umtolee kwani uk iwa mtoaji huwezi kuwa masikini.
Pia aliwaasa wakristo kuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kila wakati,pindi wakiwa katika shida na raha na sio kusubiri wakati wa matatizo ndipo waaze kumtafutaMungu,jambo ambalo halipendezi mbele za Mungu.
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment