Mwanamke aliyeasi dini nchini Sudan na kupata adhabu
ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela mjini Khartoum kwa mujibu
wa wakili wake.
Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na
mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo kuhukumiwa kifo
mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.Ataruhusiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.
Meriam aliyezaliwa na wazazi waisilamu, alihukumiwa na mahakama ya ya kiisilamu.
'Mijeledi miamoja'
Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiisilamu ambayo inasema kuwa mwanamke musilamu hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
Kwa kosa hilo, jaji alimuhukumu adhabu ya mijeledi miamoja, adhabub ambayo itatelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na kujifungua.
Bi Ibrahim alilelewa kwa njia ya kikristo , dini ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muisilamu hakuwepo katika maisha yake tangu utotoni.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International, alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Zinaa mwezi Agosti mwaka 2013, na mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini Februari 2014 aliposema kuwa yeye ni mkristo wala sio muisilamu.
Sudan ina idadi kubwa ya waisilamu ambao wanafuata sheria za kiisilamu.
BBC
No comments:
Post a Comment