Wafanyakazi wa Ujerumani Mashariki wakijenga Ukuta wa Berlin, Novemba 2, 1961.
Huu ndio ukuta wa Berlin kama ulivyokuwa unaonekana kutoka Berlin Magharibi
Mnamo Jumamosi, 12 Agosti, 1961, viongozi wa Ujerumani Mashariki (GDR) walihudhuria sherehe mjini Döllnsee, kaskazini mwa Berlin Mashariki. Hapo ndipo Katibu wa Kwanza wa chama cha Socialist Unity Party na mwenyekiti wa Baraza la Taifa la GDR Walter Ulbricht aliposaini amri ya kufunga mpaka baina ya Berlin Mashariki na Magharibi na kujenga ukuta.
Usiku wa manane, polisi na vikosi vya kijeshi vya Ujerumani Mashariki vikaufunga mpaka na asubuhi ya Agosti 3, mpaka na Ujerumani Magharibi ulikuwa umefungwa kabisa. Ukuta ukajengwa ukiwa na urefu wa kilometa 156 kwenye maeneo matatu, na kilometa 43 baina ya Berlin Mashariki na Magharibi.
Lakini baada ya mabadiliko ya kisiasa, hatimaye ukuta huo ukavunjwa. Inaelezwa kwamba ukuta huo ulivunjwa Novemba 9, 1989, lakini kwa hakika ukuta huo haukubomolewa wote katika kipindi hicho.
Kuvunjwa kwa ukuta huo ndiko hatimaye kukazaa muungano wa Ujerumani Magharibi na Mashariki mnamo Oktoba 3, 1990.
No comments:
Post a Comment