Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Meru
KANISA la T A G Patmo Nkoanekoli lililopo wilayani Meru mkoani Arusha limeweka mikakat mbalimbali ya kuombea uchaguzi wa taifa la Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2015.
Aidha uamuzi huo wa kufanya maombi ambayo yanafanyika kila mwanzo wa mwezi ili kuweza kuraishsisha uchaguzi huo wa wabunge pamoja na madiwani wa Kata zote.
Akizungumza kanisani hapo kwenye ibada ya siku ya jumapili ambayo iliongozwa na neno la mungu la kuwahimiza wakristo kutojiinua mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Japhet Nanyaro alisema kuwa utararibu huo utaweza kuwasaidia sana taifa.
Nanyaro alisema kuwa,maombi hayo ambayo yanafanywa na kanisa hilo yanalenga sehemu mbalimbali ambazo ni muhimu sana kwenye maisha ya kiroho ya Mkristo wa sasa.
Alitaja kuwa wakati wa uchaguzi na kampeni mbalimbali za nchi panakuwa na roho lukuki za kishetani ambazo zinaibuka ambapo pia wakati mwingine roho hizo husababisha hata baadhi ya damu ambazo hazina hatia kuweza kuibuka na kufanya kazi.
Aliongeza kuwa mbali na roho hizo kuweza kuibuka lakini pia wakati mwingine kuna kuwa na maroho ya kuwanyima haki wanyonge hasa wale ambao wameitwa na Mungu kutokana na watu ambao wapo kuweza kutumia vyeo vyao kuiba haki.
"Sisi tunatamani sana kuona kuwa Uchaguzi wa mwaka 2015 unakuwa ni mwaka wa baraka kwenye uchaguzi na ndio maaana kuanzia sasa tumeanza zoezi la kuomba juu ya hilo lakini pia hata juu ya viongozi kamwe wasijiinue bali wainuliwe na Mungu," aliongeza Nanyaro.
Pia aliongeza kuwa nayo makanisa mengine yanatakiwa kuhakikisha kuwa yanaweka utaratibu wa kuweza kuomba juu ya matukio ya kitaifa ndani ya nchi kwani wakati mwingine roho za kujiinua nazo zinachangia sana hata wananchi kukosa haki zao za msingi.
Mbali na hayo pia aliwataka nao wakristo kuhakikisha kuwa wanaachana na tabia ya kujiinua kutokana na vyeo vyao vya kanisa lakini hata vile vya kidunia kwani hali hiyo imesababisha walio wengi sana hasa wale wenye tabia hizo kuangamia bila kujijua.
"Nawasihi sana hakikisheni kuwa kamwe hamujiinui bali mnainuliwa na bwana mwenyewe ili msiweze kushuka ila mkjiinua na kutumia njia za mkato kwenye maisha au uongozi wa maisha yenu ya kila siku ni lazima mtapata shida na mtadhalilika sana subirini Neema ya Bwana iweze kukufika kwenye kila jambo," aliongeza Nanyaro.
No comments:
Post a Comment