Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 18 November 2016

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP MPANGO AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA FINLAND KAI MYKKANEN

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati), akipeana mkono na Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka (kulia),  baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Tanzania na Finland kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati, Biashara, Kilimo na Mawasiliano. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Finland Kai Mykkanen, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen (kulia), akizungumza katika Mkutano kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo  Kilimo, Biashara, Mawasiliano na Nishati, kati ya Tanzania na Finland . Kushoto ni Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Serikali ya Finland (kushoto) na wenyeji wao kutoka Tanzania (kulia) wakiwa katika mkutano wa pamoja wakijadili kuhusu masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Nishati, kati ya pande hizo mbili, Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe kutoka Serikali ya Finland (hawapo pichani), Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Judica Omary.


(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment