Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 November 2016

WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam jana. Mwigulu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (watano kushoto) akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika hotuba yake fupi kwa Waziri Mwigulu, alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wananchi hao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA) wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mohamed Khamis (wapili kushoto) alipokuwa akielezea jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Mwigulu alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (wa pili kushoto-mbele) akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto mstari wa mbele) mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya kutembelea ofisi za NIDA Makao Makuu na ofisi zake za usajili wa taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho, zilizopo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

*************************************************************

No comments:

Post a Comment