Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo kutoka Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Abdallah Ngoma akizungumza na wanahabari kuhusu bia ya windhoek na tamasha hilo kwa ujumla.
Mdau wa Windhoek, Kasano Jonathan akizungumzia ubora wa bia ya Windhoek.
Mkufunzi Mkuu wa Kituo cha mazoezi cha Power on Fitness cha Mwenge jijini Dar es Salaam Sas Sangandele akizungumzia umuhimu wa kufanya mazoezi.
Wadau wakipata chakula katika tamasha hilo.
Mazoezi yakiendelea.
Hapa sebene na mazoezi kwa kwenda mbele.
Hapa ni mazoezi tu kwa kusonga mbele.
Hapa ni mpango mzima wa midundo ya kamatia chini.
Wadau wa windhoek wakiwa kwenye tamasha hilo.
Hapa ni furaha tu katika tamasha hilo.
Mwonekano wa kivingine wa bia ya Windhoek katika chupa mpya.
Mazoezi yakiwa yamepamba moto.
Na Dotto Mwaibale
WADAU wa mchezo zaidi 150 wameendelea kunufaika na mazoezi ya bure ya viungo kutoka kituo cha mazoezi cha Power on Fitness cha Mwenge jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.
Akizungumza Dar es Salaam jana katika tamasha la michezo ya wazi kupitia kituo hicho, Mkufunzi Mkuu wa Kituo hicho Sas Sangandele alisema mazoezi ni muhimu sana kwa kila mtu kwani yanajenga afya na kupunguza magonjwa mwilini.
Alisema kituo hicho kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo kupitia kinywaji cha Windhoek wamekuwa wakifanya mazoezi ya wazi kwa wananchi wote bure katika viwanja vya Leaders katika wakati unaopangwa.
Alitaja michezo inayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, kufukuza kuku na mingineo mingi ambayo inafanyika katika jimu mbalimbali.
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo kutoka Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Abdallah Ngoma alisema wanajisikia fahari pale wanaoona wadau wa bia ya windhoek na wananchi kwa ujumla wanaimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi na baada ya mazoezi wanaburudika na bia ya windhoek iliyopo sokoni kwa muonekano mpya wa chupa yake huku kinywaji kikiwa kilekile.
Alisema kampuni hiyo imedhamini tamasha hilo kupitia kinywaji hicho baada ya kuona kunamuitikio mkubwa wa wananchi kwa kufanyamazoezi jambo linalowasaidia wawe na afya bora na kupoza koo kwa bia hiyo ambayo inakubalika na wengi nchini kutokana na ubora wake.
No comments:
Post a Comment