Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 20 May 2016

HIZI NI SABABU ZA AZAM KUPOKWA POINTI TATU

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepitia marejeo ya uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) kuipoka pointi zake ilizovuna kutoka mchezo Na. 156 dhidi ya Mbeya City ya Mbeya katka mchezo uliofanyika Uwanja wa sokoine mjini Mbeya.
Katika Kamati Maalumu ya TFF iliyoketi ndani ya saa 72, chini ya sekretarieti ya TFF na Bodi ya Ligi, iliyoketi Mei 17, 2016 iliipokea marejeo (revision letter) ya Azam kuhusu kupokwa pointi hizo iliamua kuingiza suala la Azam kama ajenda na kuangalia sababu za bodi kufikia uamuzi huo.Kamati ilibaini kuwa mchezaji Erasto Nyoni alikuwa na kadi tatu za njano ambazo ya kwanza aliionywa katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans uliofanyika Agosti 22, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kadhalika kamati ilibaini mchezaji huyo wa Azam FC alionyeshwa tena kwa mara ya pili katika mchezo Na. 4 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons uliofanyika Septemba 12, 2015 kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Pia, Nyoni wa Azam FC alionywa tena kwa kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo Na. 152 uliofanyika Mkwakwani mjini Tanga, uliofanyika Februari 14, 2016 hivyo ilibidi mchezaji huyo asimame mchezo Na. 156 wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City, uliofanyika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, lakini alichezeshwa na ndipo adhabu inapoiangukia Azam.
Mchezo Ngao ya Jamii unahusishwa kwa sababu za kanuni 16 (7) ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayosema: “Vitendo vya utovu wa nidhamu na ukiukwaji mwingine wa taratibu za mchezo katika mchezo wa Ngao ya Jamii utachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni hizi ambapo uamuzi wowote dhidi yake utakuwa na uhusiani wa moja kwa moja na Ligi Kiu, na mechi za ligi zinazohusisha timu husika.”
Katika kutafuta marejeo ya adhabu hiyo, Azam waliiandikia barua TFF wakisema mchezaji huyo alimaliza adhabu yake kwa kutocheza mchezo dhidi ya Yanga, Dar es Salaam kabla ya kwenda Mbeya na hivyo Erasto hakuwa na adhabu hiyo ambayo imeigharimu timu hiyo.
Awali TPLB iliinyang'anya ushindi wa Azam ambao ulikuwa ni wa pointi tatu na mabao matatu uliyovuna dhidi ya Mbeya City kutokana na kumtumia mchezaji Erasto Nyoni kwenye mechi hiyo wakati akiwa na kadi tatu za njano. Azam walipinga hatua hiyo.
TPBL ilifanya uamuzi huo, kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.


No comments:

Post a Comment