FRANK MVUNGI- Maelezo
Serikali imejipanga
kuimarisha kituo cha Jimolojia kilichopo Jijini Arusha ili kufundisha na
kuzalisha vijana wa kitanzania ili waweze kusanifu na kung’arisha madini ya
vito.Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna
wa Madini Mhandisi Ally Samaje wakati wa
mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa tathmini ya maonesho ya tano ya
kimataifa ya madini ya vito yaliyofanyika jijini Arusha mwezi Aprili 2016.
“Tayari
vijana wa kike 29 wameshapatiwa mafunzo ya miezi 6 ya ukataji wa madini ya Vito
kwenye kituo chetu cha Jimolojia na Wengine 18 wanaendelea na mafunzo ya miezi
6 yaliyoanza mwezi machi 2016” alisisitiza Samaje
Akifafanua zaidi
Mhandisi Samaje amesema Serikali ya awamu ya tano inayo dhamira ya dhati katika
kuwainua vijana wa kike kwa kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ukataji wa
madini na kuyaongezea thamani ili wachangie katika kukuza uchumi wa Taifa
kupitia sekta ya madini.
Aidha Samaje
amebainisha kuwa Serikali inaompango wa kuanzisha ukanda maalum wa uwekezaji
(EPZ) katika eneo la Mererani ambapo shughuli za biashara ya madini na
uongezaji thamani ya madini ya Tanzanite zitakafanyika kwa uhuru na uwazi.
Pamoja na
juhudi hizo Serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa Madini nje
ya nchi yakiwemo Tanzanite kwenye viwanja vya ndege na kwenye migodi ambapo
madini yanazalishwa.
Pia Samaje
alitoa wito kwa wachimbaji na wananyabiashara wa madini nchini kuzingatia
Sheria zilizopo wakati wa kufanya shughuli zao ili waweze kuchangia katika kukuza uchumi wa
Taifa.
Wizara ya
Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa madini
Tanzania (TAMIDA) iliendesha maonyesho ya tano ya kimataifa ya Madini ya vito
yaliyofanyika jijini Arusha Mwezi April,2016.maonyesho haya hufanyika kila
mwaka Jijini Arusha na kukutanisha washiriki mbalimbali wakiwemo
wachimbaji,wafanyabiashara wa madini wa ndani na nje,na wataalam mbalimbali
wenye uzoefu wa shughuli za madini ya vito.
No comments:
Post a Comment