Emmanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego
KUFUNGIWA
NA KUPIGWA MARUFUKU KWA WIMBO WA ‘PALE KATI PATAMU’ WA MSANII EMMANUEL
ELIBARIKI ‘AKA’ NEY WA MITEGO
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale kati patamu’ ulioimbwa na Msanii Ney wa
Mitengo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili.
Msanii huyu amekuwa na tabia na
mienendo yenye kuchafua Sekta ya Sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na
kufanya maonesho yenye kukiuka maadili. Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha
utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa
kada mbalimbali.
Ieleweke kwamba kwa mujibu wa
kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa
jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa
jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.
ikumbukwe kwamba BASATA limeshamuita
na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi
zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa
hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika
na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye
kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu
ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati patamu ambao uko mitandaoni ukipambwa
na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama.
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia
wasanii wachache ambao wanataka kuigeuza tasnia ya sanaa na wasanii genge la
wahuni wasio na staha na wanaojipanga kuibomoa jamii. BASATA linapenda kueleza
ya kufuatayo
·
BASATA linatamka kuwa limeufungia
wimbo huu rasmi kutumika kwa namna yoyote ile.
·
Aidha pamoja na adhabu ya kufungia
wimbo huu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha, BASATA linawataka Wasanii
wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapotengeneza kazi zao.
SANAA NI KAZI, TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey Mngereza
KATIBU
MTENDAJI
No comments:
Post a Comment