Nelly Mwangosi (kushoto) akikbidhiwa mkataba wa nyumba aliyoshinda kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers.
HIVI karibuni aliyeibuka mshindi wa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyoendeshwa na Global Publishers Ltd kwa muda wa miezi sita, alikabidhiwa mjengo wake wenye thamani ya mamilioni, uliopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Nelly Mwangosi, mama wa watoto wawili mwenyeji wa mkoani Iringa, aliambatana na mumewe Karoli Stephen Magani, pamoja na mtoto wao Emmanuel, katika makabidhiano hayo.
Nelly Mwangosi akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani)
Hapa chini ni mahojiano aliyofanya na gazeti hili baada ya kukabidhiwa nyumba hiyo.
MPAKA HOME: Unaionaje nyumba?
NELLY: Aisee ni nzuri sana, nimeipenda, ninamshukuru Mungu kwa rehemu zake hata mimi kuimiliki.
MPAKA HOME: Unayazungumziaje mazingira yanayoizunguka nyumba?
NELLY: Mazingira ni mazuri, yanavutia na isitoshe ni tulivu sana.
MPAKA HOME: Picha gani ulikuwa unaijenga kichwani kabla ya kufika hapa mjengoni?
NELLY: Kwa kweli ni vigumu kuielezea lakini nilikuwa ninaamini ni nyumba ya kisasa kwa sababu picha zake nilikuwa ninaziona kwenye komputa ya mume wangu na kwenye magazeti.
MPAKA HOME: Tofauti ya mazingira ya ndani na hapa na nyumbani kwako ni yapi?
NELLY: Nyumba hii imejengwa kisasa kuliko ile ya nyumbani Iringa, kama unavyoona sebule ni kubwa, kuna jiko, chumba kikubwa na hata samani ni za gharama sana kulinganisha na nyumbani kwangu.
MPAKA HOME: Mpango wa kuhamia hapa uko vipi?
NELLY: Mpango upo, kiukweli nitahamia Dar ‘soon’ maana muda mrefu tulipenda kuishi hapa jijini lakini hatukuwa na kiwanja wala nyumba, kwa hiyo kutokana na bahati hii nafikiri nitazungumza na mzee ili tuhamie hapa haraka iwezekanavyo.
MPAKA HOME: Vipi kama mzee akikataa?
NELLY: Sidhani kama anaweza kukataa, tutahamia tu.
MPAKA HOME: Mpaka umeshinda inamaanisha wewe ni msomaji mzuri wa magazeti yetu, unapenda kusoma habari gani?
NELLY: Hadithi, habari na mambo mengi ya kuelimisha na kuburudisha.
MPAKA HOME: Una neno gani kwa Watanzania kufuatia ushindi wako?
NELLY: Sina zaidi ya kuwaambia kuwa imani ni kitu muhimu sana katika kila kitu mtu anachofanya. Mimi nilianza kushiriki hizi droo za Shinda Nyumba nikiamini mshindi ni mtu yeyote yule ambaye bahati itamuangukia na kweli nilishiriki kwa moyo mmoja na nimefanikiwa kuibuka mshindi.
No comments:
Post a Comment