Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa amevaa mtungi wa hewa safi na
salama ambao utumiwa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pindi anapokosa
hewa wakati wa tukio la uzimaji moto au maokozi. Kushoto ni Mrekebishaji wa
Vifaa vya Kupumulia wa Jeshi hilo, Sajini Paul Mwenda. Wapili
kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishna Jenerali Thobias Andengenye. Masauni
aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya
kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini
Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwaangalia Askari wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji wakionyesha jinsi wanavyofanya uokoaji wakati ajali mbalimbali
zinapotokea nchini. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani
ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha
Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiangalia Askari wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji wakizima moto wakati tukio la moto linapotokea. Masauni aliongoza
msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza
kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akipokea maelezo kutoka
kwa Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni Kamanda wa
Jeshi hilo Mkoa wa Ilala, Ully Mbuluko jinsi chumba cha mawasiliano
kinavyopokea miito mbalimbali ya matukio ya majanga. Masauni aliongoza msafara
wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za
Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Mabalozi wa Usalama
Barabarani pamoja na Askari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara
baada ya Naibu Waziri huyo na Mabalozi hao kuonyeshwa shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Jeshi hilo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka Mabalozi hao
waendelee kushirikiana na Wizara yake katika kupambana na ajali nchini. Tukio
hilo lilifanyika katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es
Salaam. Wapili kushoto (meza kuu), Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias
Andengenye.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akimsikiliza Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (kushoto)
alipokuwa anatoa maelezo jinsi Jeshi lake linavyofanyakazi katika matukio
mbalimbali ya uzimaji moto au uokozi yanapotokea nchini. Masauni aliongoza
msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza
kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es
Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment