Karia aliyefunga kozi hiyo na kugawa vyeti kutoka FIFA kwa wahitimu 48, alisema hayo jana kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa hafla ya kufunga kozi hiyo iliyochukua takribani siku tano ambako sehemu ya mafunzo hayo ilikuwa ni kusoma baadhi ya marekebisho kwa msimu wa 2016/17.
“Tuna matagemeo makubwa kutoka kwenu, lakini nasema mfikirie kusaidia wenzenu ili kama si kumaliza matatizo kwenye soka basi yapungue, nasisitiza msiwe wachoyo, fundisheni wengine na muwape hamasa,” alisema Karia kwa niaba ya Rais Jamal Malinzi ambaye kwa sababu za majukumu, hakudhuria hafla hiyo.
Karia ambaye aliishukuru FIFA kuendelea kutoa kozi nyingi nchini, alisema kwamba tayari Tanzania imefaidika kwa kozi za makocha na makamishna, lakini akaagiza Idara ya Ufundi ya TFF chini ya Kocha Mkongwe, Salum Madadi kutoa mafunzo hayo kwa viongozi wa klabu na waandishi wa habari ambao ni sehemu kubwa ya familia ya mpira wa miguu.
Alisema kwamba umahiri wa makocha utakuwa chachu ya mafanikio ya soka la Tanzania kwa kutoa waamuzi bora watakaokuwa wakipata nafasi kubwa ya kuchezesha michezo mbalimbali ya mpira wa miguu.
“Mkifanya vibaya kwenye mashindano, mtakuwa mmejiharibia wenyewe na pia kupoteza sifa ya nchi,” alisisitiza.
Kozi za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania ilianza Julai 25, 2016 ambako iliendeshwa na wakufunzi Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini, Mark Mzengo kutoka Malawi na Felix Tangawarima wa Zimbabwe.
Leo Julai 29, 2016 limeanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.
No comments:
Post a Comment