Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe, Elizabeth Oming'o (kulia), akitoa historia fupi ya hospitali hiyo kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo (wa pili kulia), kupokea msaada wa mashuka 375 yenye thamani ya sh.milioni nane kutoka Mfuko wa Pensheni wa LAPF katika hafla ya makabidhiano yaliyofanyika juzi hospitalini hapo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Madiwani wa Halmshauri hiyo, Jnady Chakachaka na Mwenyekiti wa Huduma za Jamii wa Kisarawe, Abel Mudo.
Wafanyakazi wa kada mbalimbali wa hositali hiyo wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa mashuka hayo.
Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii wa Halmshauri hiyo, Abel Mudo, akijitambulisha.
Katibu wa Madiwani wa Halmshauri hiyo, Jnady Chaka chaka (kushoto), akijitambulisha.
Katibu wa Waziri Jafo, Eleuter Kihwele (kushoto), akijitambulisha.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (kushoto), akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo, akisisitiza jambo. Kutoka kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Juma Kanena, aliyemwakilisha OCD katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kisarawe, Patrick Allute na Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii wa Halmshauri hiyo, Abel Mudo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo (kushoto), akisisitiza jambo kwenye hafla hiyo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (katikati), akimkabidhi Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo (wa pili kushoto), msaada wa mashuka 375 yenye thamani ya sh.milioni nane kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo juzi. Kutoka kushoto ni Mganga wa hospitali hiyo, Elizabeth Oming'o, Mwenyekiti wa Huduma za Kijamii wa Halmshauri ya Kisarawe, Abel Mudo.
Waziri Jafo (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wilaya hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Kisarawe
MFUKO wa Pensheni wa LAPF, umetoa msaada wa mashuka 375 yenye thamani ya sh.milioni nane kwa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.
Hafla ya kukabidhiana mashuka hayo ilifanyika juzi katika hospitali hiyo kati ya Mbunge wa Kisarawe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Tamisemi, , Suleiman Jaffo na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo
Mlowe alisema wametoa msaada huo baada ya kutambua wadau wakubwa wa hospitali hiyo ni wateja wao na wananchi wenye kipato cha chini.
Alisema wanaofika kupata huduma katika hospitali hiyo ni wadau wao hivyo watashirikiana bega kwa bega kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapofuata huduma.
Mlowe alisema walipokea maombi ya kuiwezesha hospitali hiyo kutokana na changamoto zilizopo hivyo wameona ni vyema wakatoa mashuka ambayo yatasaidia kupunguza uhaba uliopo sasa.
"Suala la afya kwetu sisi ni kipaumbele cha kwanza hivyo ili kupata wanachama bora na wenye afya ni lazima sekta hii iwezeshwe," alisema Mlowe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (OR Tamisemi), Suleiman Jafo alisema kuimarisha Sekta ya Afya ni pamoja na kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Alisema hospitali ya Kisarawe ina wataalam wengi wa afya japokuwa inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji kutatuliwa.
Jafo alisema ni vyema vifaa vilivyopo vikatumika kwa walengwa ambao ni wananchi na kuacha ubaguzi wakati wa utoaji tiba.
Mganga wa Wilaya hiyo, Elizabeth Oming'o alisema wanakabiliwa na changamoto ya vifaa tiba katika hospitali hiyo na vituo vya afya.
Alisema hospitali hiyo no ya muda mrefu hivyo miundombinu yake inahitaji pia ukarabati.
Dk.Elizabeth alisema kwa muda mrefu mashine ya Ultra Sound imeharibika bado haijafanyiwa matengenezo jambo linalowalazimu wagonjwa wao kupima nje ya hospitali.
Hata hivyo alisema uhaba wa wafanyakazi wa kada mbalimbali katika hospitali hiyo imesababisha huduma kushindwa kutolewa kwa wakati.
"Uhaba wa watumishi wa kada mbalimbali kwetu ni changamoto hivyo tayari tumeomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi," alisema Dk.Elizabeth.
Alisema hospitali hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa mashuka 1200 ambapo hadi sasa wamepokea msaada wa mashuka 475 ambayo kati ya hayo 100 yalitolewa na Mamlaka ya Bandari Tanzania na mengine 375 kutoka LAPF.
No comments:
Post a Comment