Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akimfafanulia jambo Mkuu wa
Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) wakati wa ziara
yake nchini pamoja na ujumbe alioambatana nao walipokutana na Waziri huyo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali
ya kupambana na uhalifu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (katikati) akimsikiliza Mkuu wa
Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) alipokuwa
akimfafanulia jambo kuhusu masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. IGP Kachama
na ujumbe wake yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi. Mazungumzo hayo
yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimuaga Mkuu wa Jeshi
la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama mara baada ya mazungumzo yao
ofisini kwake jijini Dar es Salaam. IGP Kachama yupo nchini kwa ziara ya
kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment