Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Afisa
Uhusiano wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bi. Edna John wakati alipotembelea
ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
Mtendaji
Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa
mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipokagua ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo
la Bunju B jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipokagua ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo
la Bunju B jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua baadhi ya
miundombinu iliyopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za wafanyakazi zilizopo
Bunju B jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi
wa ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es
salaam.
Meneja
Mradi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania Arch.Humphrey Killo akifafanua mchoro
wa ramani ya ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam
katika barabara ya Sam Nujoma,wa kwanza kushoto ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga .
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa
Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch.Elius Mwakalinga wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa
Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Muonekano
wa awali wa ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Muonekano
wa nyumba za wafanyakazi nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es
salaam.
PICHA
ZOTE NA BENJAMINI SAWE-MAELEZO
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) kuhakikisha wanakamilisha haraka miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi
wa umma zinazojengwa nchini kote.
Ameyasema hayo mara baada ya kukagua mradi
wa ujenzi wa nyumba za watumishi 851 zilizopo eneo la Bunju "B"
ambazo zipo katika mpango wa Wakala wa kujenga nyumba 10,000 kwa ajili ya
watumishi wa umma na kuona hatua zilizofikiwa.
Waziri Mbarawa amesema kukamilika kwa
ujenzi huo kutawawezesha watumishi wa umma kupata makazi yaliyobora na ya
uhakika na hivyo kuiwezesha tba kujipatia marejesho ya fedha walizowekeza kwa
wakati.
"Bora mjenge nyumba kidogo lakini
zinamalizika kuliko kujenga nyumba nyingi kwa wakati mmoja lakini
hazimaliziki", amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amewatala TBA kuhakikisha
wanamaliza ujenzi wa miradi ya nyumba na majengo kwa wakati na kuziuza ili
kupata faida itayowawezesha kujenga nyumba nyingine badala ya kuwa na miradi
mingi ya ujenzi ambayo haijakamilika.
Ameitaka TBA kubadilika kimtazamo na
kiutaalamu kuanzia watendaji hadi wafanyakazi wake na kuanza kufanya kazi kwa
malengo ili kuwezesha kukabiliana na ushindani wa kibiashara wa majengo hapa
nchini.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa
amekagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam uliopo barabara ya Sam Nujoma ambapo ameridhishwa na kasi ya maendeleo
ya mradi huo.
Amewataka wakala huo kuhakikisha
wanakamilisha kwa wakati na kwa kuzingatia viwango na ubora vilivyowekwa ili
kuweza kuondoa changamoto ya makazi inayowakabili wanafunzi hao.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa TBA Arch.
Humphrey Killo amesema ujenzi wa mradi wa mabweni ya wanafunzi utahusisha
ujenzi wa vyumba 960 vyenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 3,840 na
ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi sita.
Naye Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Elius
Mwakalinga amemhakikishia waziri kuwa wakala wake utafanya kazi usiku na mchana
ili kukamilisha kwa wakati mradi huo kwa kuwa inayo uwezo wa kiteknolojia wa
ujenzi wa miradi ya majengo hapa nchini.
"Kuonyesha kuwa uwezo wa kufanya
miradi kama hiyo tunayo, tutaikamilisha kwa wakati na viwango stahili ili
wateja wapate thamani ya pesa watakayolipa", amesema Arch. Mwakalinga.
Zaidi ya nyumba 10,000 za makazi ya
watumishi wa umma zinatarajiwa kujengwa na kuuzwa katika mradi wa Bunju
"B" ikiwa ni mkakaati wa Serikali kuwawezesha watumishi wa umma
kupata nyumba bora kwa bei nafuu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment