Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 15 December 2016

MICHEZO YA TANO YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA YATIMUA VUMBI TANGA


Tanga, MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kwenda kasi ya  Serikali ya awamu ya Tano.
Akifungua michezo ya Tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga jana, Kakoko, alisema kila mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.
Alisema kasi hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na kuwa kivutio kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao bandari za Tanzania.
Michezo hiyo inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.





No comments:

Post a Comment