Fundi
Martin Justine akitengeneza paa la kisima cha maji safi kinacho jengwa
Soko la Madenge Temeke jijini Dar es Salaam kwa nguvu za
wafanyabiashara. Ujenzi wa kisima hicho umegharimu sh.milioni 5.6.
Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
Katibu
Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala'
akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
Katibu
Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akinawa
maji yanayotoka katika kisima hicho ambacho ujenzi wake umekamilika kwa
asilimia kubwa.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYABIASHARA
katika Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam
wamejenga kisima cha maji salama chenye thamani ya sh.milioni 5.6 kwa
kutumia nguvu zao na fedha za ushuru wanaolipa.
Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Katibu
Mkuu wa Soko hilo Shaban Malonji 'maarufu kama Wailala' alisema umoja
walionao wafanyabiashara katika soko hilo ndio uliofikia maazimio ya
kujenga kisima hicho chini ya viongozi wao.
"
Binafsi napenda kuwapongeza wafanyabiashara wa soko letu kwa kuwa na
umoja ambao umefanikisha kukamilisha ujenzi wa kisima hiki ambao
utakamilika rasmi mapema wiki hii" alisema Malonji.
Malonji
alisema kwa muda mrefu changamoto yao ilikuwa ni kukosa maji sokoni
hapo ndipo walipokaa na wafanyabiashara wa soko hilo na kufikia maazimio
ya kujenga kisima hicho ambacho kitakuwa kikitoa huduma ya maji sokoni
hapo.
Alisema
fedha za ujenzi wa kisima hicho zimetokana na ushuru wanaotoa
wafanyabiashara hao na fedha zinazopatikana baada ya kulipa huduma ya
choo cha kulipia pamoja na fedha za ushuru asilimia 10 wanazopewa na
Manispaa.
No comments:
Post a Comment